Blogger Widgets

Wednesday, September 11, 2013

MAMA MMOJA AIFICHA MAITI YA MTOTO WAKE KWA MIAKA 18 KISA ANAMPENDA SANA.

 
Mama ambaye mtoto wake wa kiume alifariki miaka 18 iliyopita amemuhifadhi katika pombe na kuficha mwili wake kwenye sehemu ya chini ya makazi yake ambako amekuwa akimhudumia muda wote tangu wakati huo... yote hayo ili kijana wake aweze kuona anavyompenda.

Tsiuri Kvaratskhelia ameuhifadhi mwili wa Joni Bakaradze uliozikwa ndani ya jeneza la mbao sambamba na nyumba hiyo ya familia mjini Georgia, mashariki mwa Ulaya.

Lakini licha ya kuwa amekufa mwaka 1995, mwili wa kijana huyo mwenye miaka 22 umebaki ukiwa umekaushwa damu kikamilifu, shukrani kwa mama yake aliyeonesha mapenzi ya kweli na uangalizi wa karibu.
 

Na kila mwaka katika maadhimisho ya siku yake ya kuzaliwa mama huyo amekuwa akimbadilisha nguo - hadi miaka minne iliyopita pale uozo hatimaye ulipofanya kazi hiyo kushindikana.

"Alitaka mtoto wake kumwona kwa namna hiyo," alielezea. "Naamini kutokea hapo mtoto huyo alianza kumpenda baba yake."

Pia kuna dirisha dogo la kutazamia kwenye sehemu hiyo ya chini hivyo familia, marafiki na wapita njia wanaweza kuona jinsi anavyoendelea.

Mama Kvaratskhelia amejifunza zaidi kuliko mbinu chache kumfanya mtoto wake huyo awe na mwonekano mzuri.

"Usiku mmoja niliota pale sauti fulani iliponieleza kumshughulikia Joni kwa kumwagia pombe hivyo kutokea hapo nimekuwa nikitumia mashuka yenye unyevu yaliyozamishwa kwenye pombe kuhifadhi mwili wake," alisema. "Hutakiwi kuuacha mwili huo bila mashuka hayo wakati wa usiku sababu ngozi itabadilika na kuwa nyeusi kama makaa ya mawe."

Aliongeza: "Kwa miaka 10 nimekuwa nikimbadilisha nguo zake wakati wa maadhimisho ya siku yake ya kuzaliwa. Miaka minne tu iliyopita ndio sikuweza kufanya hivyo.

"Alikuwa mtu safi, mume mwema, si kama hivi alivyo sasa."

Lakini sasa Joni, ambaye sababu za kifo chake hazijafahamika, hatimaye anaanza kuharibika tangu maradhi kumzuia Mama Kvaratskhelia kumpatia matunzo ya kila siku anayohitaji.

"Nilikuwa naumwa hivi karibuni na sikuweza kuhudumia mwili wake," alisema. "Hiyo ilikuwa na athari kwake.

"Mtoto wangu ni anavutia. Nitakapoanza kutumia mashuka hayo ngozi yake itakuwa angavu tena na kila kitu kitakuwa kama kawaida."




 

0 comments:

Post a Comment