Kuna
watu ambao katika maisha yao ya kila siku hawana tabia ya kunywa maji
mara kwa mara . Hii ni kutokana na kuona kero kwa kunywa maji kila
wakati au kuona uvivu wa kubeba chupa za maji au kulazimika kufuata
mahali ambapo maji yanapatikana lakini kubwa kuliko zote kati ya sababu
hizo ni kutofahamu umuhimu wa kunywa maji mara kwa mara katika maisha ya
afya ya mwanadamu.
Maji
ni sehemu muhimu ya maisha ya mwanadamu na yana machango mkubwa sana
katika afya ya mwili na kama yakinywewa ipasavyo yanaweza kukuepusha na
magonjwa mengi ambayo yatakufanya uishi maisha marefu .
Maji yanakufanya uendelee kuonekana mdogo.
Maji
yanafanya ngozi yako iwe na vimeleo au mabaki muhimu ya maji muda wote
na hivyo kuondoa adha ya ngozi kuharibika kutokana na umri mkubwa . Maji
kiasilia hurutubisha ngozi huku ikijazia mistari ambayo huondoa
makunyanzi na kuifanya ionekana kuwa nyororo na laini.
Unywaji wa maji huondoa Msongo wa mawazo.
Unaweza
ukashindwa kuamini jinsi gani maji yana mchango kwenye afya ya
saikolojia yako lakini ile sauti ya maji yakiwa yanachuruzika inaweza
kutuliza mawazo yako na kuondoa msongo wa mawazo .
Maji yasaidia kupunguza na kuponya mafua .
Unywaji
wa maji husaidia kuondoa mafua kwa wale wenye allergy ya vumbi na
uchafu na pia kunawa mikono mara kwa mara kwa maji masafi kunasaidia
kuua vijidudu ambavyo huwafanya watu kupata mafua mara kwa mara .
Maji yasaidia nywele.
Kwa
wale wadau wa masuala ya urembo hasa kina dada zaidi ya kuritubisha
ngozi maji husaidia kung’arisha nywele . Kuosha nywele kwa maji ambayo
hayajachemshwa kwa kutumia virutubisho vya nywele vya kutengeneza kama
vile shampoo na mafuta maalum aina ya conditioner yanazifanya nywele
kuwa thabiti zaidi na kuondoa uwezekano wa kungoka hovyo hovyo huku
zikiwa na mn’gao .
Ngozi ya mwili husaidiwa sana na maji.
Zaidi
ya ngozi ya uso maji ni muhimu kwa ngozi ya mwili kwa ujumla . Wakati
wa kuoga maji ya moto au vugu vugu hufanya ngozi ya mwili kuwa nyororo
na yenye afya zaidi , maji husaidia kuondoa ukavu ambao huondoa mvuto wa
asili wa ngozi na kuipa afya kwa ujumla .
Maji husaidia kupunguza uzito wa mwili.
Kwa
wale wenye matatizo ya uzito ambayo wakati mwingine yanaweza yakawa
hatari kwa afya yako kwa kusababisha matatizo kama Presha ,kisukari na
magonjwa ya moyo maji yanaweza kuwa kimbilio lako. Kwa kujibu wa utafiti
, watu wazima wanaokunywa glasi nane za maji kwa siku yaani angalau
glass mbili kwa kila baada ya saa kadhaa hasa kabla ya wakati wa kula
wanajikuta wakila chakula kidogo na hivyo kufanya mwili wako kupata
chakula kile kile kinachohitajika na mwili wako na hivyo kuondoa
uwezekano wa mwili wako kulimbikiza chakula kinachofanya uzito wako
uendelee.
Maji huisaidia akili kufanya kazi vizuri .
Mwili unapokosa maji tatizo pekee sio mtu kuhisi kiu wakati
mwingine ubongo huhisi kuchoka kirahisi na haraka pale ambapo mtu
hajanywa maji muda mrefu . Hisia kama hasira , uchovu wa akili ,
kuchanganyikiwa humtokea mtu kirahisi wakati akiwa hajanywa maji muda
mrefu na wakati mwingine hata kichwa huuuma sana lakini suluhisho la
yote haya ni kunywa maji mara kwa mara .
Muwasho wa koo.
Muwasho
wa koo unaotokana na allergy au mafua hutibiwa na maji , mtu anapopata
tatizo hili suluhisho la haraka ni kusukutua maji yenye chumvi lakini
kuepsuah tatizo hili ni kuhakikisha koo halikauki kwa muda mrefu .
Maji husaidia kupigana dhidi ya magonjwa .
Maji
yana msaada mkubwa sana kwenye kupambana na magonjwa mwilini mwako . Ni
vizuri kunywa maji mara kwa mara kuepusha mwili wako na magonjwa . Pia
ulaji wa matunda husaidia kuupa mwili maji muhimu yanayokuwa kinga dhidi
ya magonjwa mbalimbali . Matunda kama mapapai,matikiti
maji,matango,machungwa ,ndizi,maembe yanauongezea mwili maji ambayo
yanakufanya ukae muda mrefu bila kuugua .
0 comments:
Post a Comment