Msanii wa muziki wa bongoflava, Diamond akiwakaribisha watanzania kuhudhuria tamasha hilo.
Msanii toka mwamba wa kaskazini, Joh Makini akieleza machache.
---
Na Kajunason Blog
Tamasha kubwa la “Kili Music Tour” lililoandaliwa na Tanzania Breweries Limited (TBL) chini ya nembo ya Kilimanjaro Premium Lager linahitimishwa na show kubwa ya Dar es Salaam Jumamosi hii tarehe 14 katika viwanja vya Leaders Club.
Ziara
hii kubwa ya muziki mpaka sasa imefanyika kwenye mikoa 7 nchini kote
ambapo zaidi ya wasaniii 28 wameshirikishwa ikijumuisha baadhi ya
wateule na washindi wa mashindano ya Kili Tanzania Music Awards 2013
pamoja na wasanii wengine wanaong’ara kwenye fani ya muziki nchini.
Meneja
wa Bia ya Kilimanjaro Bwana George Kavishe alinukuliwa akisema kuwa
ziara hizi ni sehemu ya juhudi za chapa ya Kilimanjaro Premium Lager
katika suala zima la kuhamasisha na kuinua muziki wa Kitanzania,
hususan, kwa wanamuziki wa nyumbani; vilevile ni tunu ya heshima kwa
watanzania kwa kuendelea kuunga mkono
bia ya Kilimanjaro.
“Kili
Music Tour 2013 ilizinduliwa na kauli-mbiu ya “Kikwetu Kwetu” ambayo ni
kampeni ya Kilimanjaro Premium Lager ya kuhamasisha hisia za uzalendo
kwa watanzania kwenye kuthamini vitu ambavyo ni vya kwetu na ni
vyakitofauti kabisa kama lugha yetu ya Kiswanglish, muziki wetu wa bongo
fleva, dansi yetu ya kiduku, kandanda yetu yenye upinzani wa Simba na
Yanga, na bia yetu ya Kilimanjaro ambayo imetengenezwa Tanzania, na
viungo vya kitanzania na watanzania kwa ajili ya Tanzania.” Alisema
bwana Kavishe.
“Ziara
ya mwaka huu ilikuwa ni kubwa kuliko zote zilizopita kwani tuliongeza
mikoa na kufikia minane kutoka mitano ya mwaka jana na tuliongeza idadi
ya washiriki wa tamasha kufikia zaidi ya 28. Vile vile tulishirikisha,
si tu washindi wa 2013 wa ‘Kili Tanzania Music Awards’ pekee, bali pia
na baadhi ya wateule wa tuzo na baadhi ya wanamuziki mashuhuri
wanaong’ara katika tasnia ya muziki.
Kwa
kuwa Kilimanjaro Premium Lager ni bia ya kizawa iliyoasisiwa Tanzania
inatambua ni kwa kiasi gani watu wetu wanajivunia upekee wa kitanzania
kama ilivyo bia yao hii na ndiyo sababu kubwa iliyotufanya tuwapeleke
wanamuziki walio bora katika fani kwenye milango ya washabiki huko
waliko mikoani kupitia mtindo wetu wa ‘Kikwetu kwetu!” alimalizia bwana
Kavishe.
Wasanii
14 watashiriki watashiriki kwenye tamasha la Dar es Salaam ambao ni:-
Diamond Platinum, Professor J, Ben Pol, Lady Jay Dee, Lynex, Roma,
Recho, Kala Jeremiah, Joh Makini, Mzee Yusuph, Mashujaa Band, Ney wa
Mitego, Ras Six na
Tip Top Connection.NA LUKAZA BLOG
0 comments:
Post a Comment