
Stori: Richard Bukos
KIOJA cha mwaka kilitokea Jumatano wiki hii katika Mahakama ya Jiji ya
Sokoine Drive jijini Dar es Salaam, baada ya mkazi mmoja wa Buguruni,
Hassan Omary kujisaidia haja kubwa kizimbani wakati akisomewa shtaka
lake la uzururaji.

Mwendesha
mashitaka wa mahakama hiyo, Richard Magodi alikuwa akimsomea shtaka
hilo, mbele ya Hakimu Mfawidhi, William Mutaki na alipotakiwa kukiri au
kukanusha kosa lake, mtuhumiwa huyo alibaki kimya akiwa amemtumbulia
macho hakimu.

Katika
hali isiyotarajiwa, mtuhumiwa huyo alionekana akijikamua kama
anayejisaidia na ghafla, harufu kali ya kinyesi ikatanda mahakamani
hapo.Hakimu alitahayari kufuatia tukio hilo, kwani aliziba pua yake kwa
kutumia koti lake na kuuliza chanzo cha mtuhumiwa kufanya kitendo hicho
kortini, lakini katika hali iliyoashiria kama ni kiburi, kijana huyo
hakujibu chochote zaidi ya kutazama chini, licha ya swali hilo kurudiwa
zaidi ya mara tatu.

Kutokana
na kosa hilo ambalo liliharibu na kusimamisha karibu shughuli zote za
mahakama kwa muda, Hakimu Mutaki alimhukumu kijana huyo kwenda jela kwa
muda wa miezi sita ili kuwa fundisho kwa wengine wenye tabia hiyo.
Kana kwamba haitoshi, askari waliokuwepo mahakamani hapo walilazimika
kumchapa bakora kijana huyo ili kumlazimisha kupiga deki baada ya eneo
hilo kuchafuka vibaya kwa kinyesi kilichochanganyika na mkojo.
0 comments:
Post a Comment