Blogger Widgets

Wednesday, April 17, 2013

Angalia Picha mbalimbali za Maandalizi ya Mazishi ya Marehemu Bi Kidude.


Gari lililokuwa limeubeba mwili wa msanii mkongwe wa muziki wa tarab, marehemu Fatuma Binti Baraka 'Bi. Kidude', likiusafirisha kutoka katika Kijiji cha Kihinani na kuupeleka nyumbani kwake Rahaleo kwa matayarisho ya mazishi yatayofanyika kesho mchana katika Kijiji cha Kitumba, Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja. (Picha zote kwa hisani ya Othman Maulid wa ZanZinews)
Mwili wa marehemu ukishushwa katika gari wakat ukiwasili nyumbani kwake, Rahaleo kwa taratibu za mazishi yatakayofanyika kesho mchana na Kijiji cha Kitumba, Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja.
Ndugu, Jamaa na marafiki, wakiubeba mwili wa marehemu Bi. Kidude wakati ulipowasili nyumbani kwake, Rahaleo kwa ajili ya matayarisho ya mazishi yatakayofanyika kesho Kijiji cha Kitumba, Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja.
Mrajisi wa Baraza la Sanaa la Zanzibar, Khadija Batashi, akizungumza na waandishi wa habari jinsi alivyoupokea msiba wa msanii mkongwe wa muziki wa taraba nchini, Bi Kidude.
Matayarishi ya mazishi ya msanii wa muziki wa tarab, Bi. Kidude yakiendelea nyumbani kwake Rahaleo, mjini Zanzibar.
Mjukuu wa Bi. Kidude Omar Ameir, akiwasiliana na jamaa kwa ajili ya kuwajulisha msiba wa marehemu Bi. Kidude, baada ya mwili wa marehemu huyo, kuwasili nyumba kwake kwa ajilimatayarisho ya mazishi yatakayofanyika kesho mchana baada ya Swala ya Adhuhuri, ambapo atazikwa Kitumba.
Bi. Maryam Hamdani akilakiwa na Bi. Sihaba wakati akiwasili nyumbani kwa marehemu Bi. Kidude Rahaleo, mjini Zanzibar akiwa na majonzi.  
Waandishi wa habari wakizungumza na Mfadhili Mkubwa wa Bi. Kidude, Maryam Hamdan, kuhusiana na marehemu ambaye yeye alikuwa ni mtayarishaji na mratibu wa safari za Bi. Kidude nje ya nchi na katika matamasha mbalimbali aliyokuwa akihudhuria nje ya nchi wakati wa uhai wake.

1 comment:

  1. Ni msiba wenye majonzi na Machungu mengi kwa wale wooote walio mfahamu Bi Kidude lakini hata kwa wanaotambua mchango wake kwa taifa letu na tadhinia nzima ya muziki wa Mwambao hapa nchini, mimi niseme yeye kamaliza safari yake kwa jinsi ambavyo Allah Kamjalia kazi imepaki kwetu sisi je tutazifuata nyayo zake kwa yale mema aliyoyafanya?
    Tusiishie kulia na kuhuzunika tukizungumza na kupamba kwa maneneo Lukuki juu ya yale mema aliyoyafanya Bi Kidude pasipo kuyafuata na kuyaenzi,Nitoe Pole kwa Ndugu jamaa na marafiki woote walioguswa na msiba huu kwa namna moja au nyingine kwa kumpoteza,mama yao,dada yao,Bibi yao,nyanya yao,mtoto wao,mpendwa wao lakini Mwisho tumuombee Mungu ailaze Roho yake Mahali Pema Peponi na tutambua kuwa kazi ya Mungu haina Makosa.

    ReplyDelete