Blogger Widgets

Thursday, April 18, 2013

MSIBA WA BILIONEA BABU SAMBEKE WAZUA GUMZO,,,,VIGOGO WATAWALA MSIBANI .... TUKIO KAMILI LA MAZISHI LIPO HAPA

DSCF8833

Jamal Sambeke mtoto wa marehemu akifunga jeneza la baba yake mara baada ya watu mbalimbali kutoa heshima zao za mwisho nyumbani kwake njiro Themi Mkoani Arusha
DSCF8840
Waombolezaji wakibeba jeneza la Bilionea Babu na kuweka kwenye gari maalumu tayari kwa safari kuelekea Moshi kwa mazishiDSCF8828
Watu wakitoa heshima za mwisho
DSCF8844
Watoto wa marehemu Sia na Getrude waliovalia nguo nyeupe
DSCF8834
Jamal akifunga jeneza la marehemu Babu Sambeke
DSCF8830
Jaji Aisha nyerere msibani pamoja na mkurugenzi wa kibo palace Vicent Laswai
DSCF8832 DSCF8848
Baadhi ya magari ya kifahari yaliyofika katika msiba huo
DSCF8838
Mkurugenzi wa hoteli ya Kibo Palace Vicent Laswai akizungumza msibani mara baada ya watu mbalimbali kutoa heshima zao za mwisho

DSCF8847
Waombolezaji
Mamia ya vigogo pamoja na watu mbalimbali wafurika nyumbabi kwa marehemu Bilionea “Babu Sambeke”Ernest Sambeke eneo la njiro jijini Arusha kuaga mwili wake unaotarajiwa kuzikwa kesho nyumbani kwake eneo la Karanga mjini Moshi huku msiba huo ukiwa tofauti na misiba mingine iliyozoekeaka hapa Nchini
Marehemu,Sambeke alifariki hivi karibuni katika ajali ya ndege aliyokuwa akiiendesha na pia mmiliki wa ndege hiyo ambapo ilianguka katika eneo la Kisongo na kusababisha kifo chake Mkoani Arusha
Shughuli za kuaga mwili wa marehu zilikamilika majira ya saa 8:45 mchana huku mwili huo ukipakiwa katika gari maalumu la kifahari tayari kusafirishwa kuelekea nyumbani kwake Moshi kwaaajili ya mazishi
Taratibu za kuaga mwili wa marehemu zilianza majira ya saa 5 asubuhi huku wafanyabiashara wa madini pamoja wafanyabiashara wengine kutoka hapa Arusha na Moshi walionekana kutawala msiba huo.
Katika zoezi hilo la kuaga mwili wa mareheu Padri Florentine Mallya ambaye ni mdogo wa marehemu aliongoza misa ya kumuombea marehemu na baada ya kumaliza alitoa fursa kwa watu mbalimbali kupita mbele ya jeneza kwaajili ya kuaga mwili Ndani ya jeneza marehemu alivalishwa nguo zake za kirubani huku ,baadhi ya wanajeshi kutoka jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) walionekana jana katika zoezi la kuuaga mwili wa marehemu ambapo baadhi yao walikuwa wamevalia sare za jeshi hilo
Hatahivyo,baadhi ya watu walionekana katika hali ya kawaida huku watoto wakionekana na nyuso za huzuni mda wote
Tofauti na misiba mingine nchini watu mbalimbali walipata fursa ya kupata chakula na vinywaji mbalimbali kwa kujihudumia vikiwemo vinywaji aina ya Bavaria ambapo watu waliohudhuria zoezi hilo walionekana wakijihudumia zaidi vinywaji vya bavaria
Magari ya kifahari yalionekana kutawala msiba huo huku barabara ya njiro ikionekana kuwa na msongamano kubwa iliyosababishwa na zoezi hilo la uwagaji wa mwili
Marehemu aliacha watoto watatu ambao ni Sia,Jamal,Getruda

JAMII BLOG

0 comments:

Post a Comment