Blogger Widgets

Tuesday, April 16, 2013

Jokate na Penny wazungumzia tetesi za uhusiano kati ya Diamond na Irene Uwoya

Katika muda ambao kila mmoja alikuwa amejaribu kuamini kuwa Diamond Platnumz ameamua kutulia na mpenzi mmoja, mtangazaji wa DTV, Penniel Mungilwa, hivi karibuni kumezuka tetesi kuwa staa huyo wa ‘Ukimuona’, ameanzisha uhusiano wa kimapenzi na muigizaji wa filamu Irene Uwoya.
page
Baadhi ya magazeti ya udaku nchini yameandika habari hiyo ikiwa na picha inazowaoenesha mastaa hao wakichukua chumba kwenye hoteli ambako yalidai walienda kufanya yao.
DIAMOND3
Kufuatia tetesi hizo, Bongo5 imezungumza na mpenzi wa sasa wa Diamond, Penny ambaye amesema kwa ufupi kuwa wameshayazungumza na Diamond na wako vizuri kwa sasa lakini akasisitiza kuwa asingependa kuliongelea zaidi suala hilo.
Katia hatua nyingine, Jokate Mwegelo aliyewahi kuwa na uhusiano na Diamond amekanusha kupitia Bongo5 taarifa iliyoandikwa na gazeti moja la udaku kuwa amemcheka Irene kwa kunaswa kwenye himaya ya Diamond.
JOKATE
“Mimi hivyo vitu havinihusu na wanapenda kupata quotes zangu pasipo hitajika. I don’t know why? I don’t why wanatafuta story. That’s their life kiukweli with whatever they choose to do, more power to them,” amesema Jokate.

chanzo:  bongo5

0 comments:

Post a Comment