Blogger Widgets

Tuesday, April 2, 2013

Wema Sepetu afunguka sababu ya kumtolea Kajala mil. 13 ili asiende jela miaka mitano, “Naamini what I did is best.”


Wema sepetu ambae amemake headlines mwanzoni mwa wiki hii na kuwaacha midomo wazi watu wengi baada ya kuingia mfukoni na kutoa sh. Million 13 kumsaidia Kajala asiende jela miaka Mitano, amefunguka sababu ya kuchukua uamuzi huo ambao wengi hawakuutegemea.
Wema ameuambia mtandao wa Bongo5 kuwa hakufikiria mara mbili kuchukua uamuzi huo, na hapo amekubali usemi kuwa kutoa ni moyo.

“Kusema kweli wanasemaga kutoa ni moyo so naamini what I did is best”, alifunguka staa huyo wa Bongo Movie.

“Nimefanya kama kumsaidia rafiki yangu kama namsaidia ndugu yangu na sidhani kama ingekuwa kitu kizuri kumuona mwenzako anaingia kwenye dhamana,kwenye tabu, kwenye mateso wakati nina uwezo wa kumsaidia kwa hiyo I just did what I had to do.”

Wema sepetu ni staa wa bongo movie ambae mara nyingi media zimekuwa zikiandika habari controversial kuhusu yeye, lakini kipindi hiki Wema ameonesha moyo mkubwa na wa kipekee alionao kwa kujitolea pesa taslim sh. Million 13 kumsaidia Kajala msanii wa kuigiza ili asiende jela miaka mitano kwa mujibu wa hukumu iliyotolewa na mahakama.

Uamuzi huu wa Wema umepongezwa sana na mastaa wa muziki na bongo Movie pamoja na wapenzi wa sanaa Tanzania. Kweli kwa hili anastahili pongezi kubwa sana, she made it.
 

0 comments:

Post a Comment