Blogger Widgets

Tuesday, April 16, 2013

Style za Kanga moja laki si pesa ni kama filamu za wakubwa..ni ‘HATARI’ usiende na mtoto au mtu unaeheshimiana nae, maana duh!




Moja kati ya makundi yanayovuma sana kwa kuwapagawisha mashabiki wakiwa jukwaani ni kundi la ‘kanga moja laki si pesa’. Kundi hilo limejipatia umaarufu mkubwa sana na hivyo kupiga matamasha wakizunguka Tanzania na kila walikopita wameacha historia ya aina yake.

Lakini Kile wanachokifanya wakiwa jukwaani hakihitaji mwalimu wa nidhamu kuwa karibu nao ama jopo la kuhifadhi maadili ya taifa kushuhudia kwa sababu endapo wakishuhudia inaweza kuzua ‘msalaaa’ si kidogo. Na tukisema ingekuwa enzi za mwalimu, dah, sijui ingekuwaje.....!
 
Style wanazocheza wakiwa jukwaani naweza kuthubutu kusema ni kama movie za wakubwa kwa asilimia kadhaa, na kwa ushauri wa haraka na muhimu ni kwamba watoto ama watu wanaoheshimiana na kuoneana aibu hawashauriwi kabisaa kushuhudia pamoja shangwe hizo za Kanga Moko laki si pesa, ikiwa hivyo mnaweza kupoteana ukumbini kukwepa aibu wakati watu ndo wanazidi kushangilia.

Ipo mitindo mingi ya kushtua wanayoicheza, lakini kati ya hiyo huu wa kumwagiwa kilevi sehemu za faragha kisha kuchezesha maungo yaliyolowana na kuonekana mithili ya karatasi iliyomwagiwa mafuta ya taa na kilaza ili aitumie kuchora kwa urahisi ramani iliyowekwa chini ya karatasi hiyo kwa kufuatisha tu, imetisha!! Hapa naweka kalamu chini nisigusie sana sentensi  hii‘Maadili ya Kitanzania yako wapi?’

Jionee mwenyewe baadhi ya picha za ‘kanga moko’ zilizochukuliwa huko Bukoba wakiwa wanamsindikiza Diamond Platinumz kuwapa shangwe wakazi wa Bukoba, show iliyoweka historia ya aina yake mjini humo.








Wataalam wa mambo wanakwambia 'DON'T TRY THIS AT HOME'.

0 comments:

Post a Comment