Blogger Widgets

Tuesday, April 2, 2013

Lady Jay Dee achafukwa na roho na kuanzisha kituo chake cha Radio soon, kitaitwa ‘Kwanza FM’.

Baada ya kuwasha moto wenye joto hasira kupitia mtandao wa kijamii wa twitter akiuelekeza kwa kituo kimoja cha radio ‘radio ya watu’ kwa takribani siku 4 hivi. Sasa Lady Jay Dee, Binti Komando ametangaza rasmi kupitia account yake ya twitter kuwa anaanzisha kituo chake mwenyewe cha radio hivi karibuni.

Tweet yake inasomeka, “Kwanza Fm coming soon. Yangu Mwenyewee”. Hii inamaanisha kuwa mmiliki wa ‘Kwanza Fm’ ni yeye binti komando, Lady Jay Dee ambae kupitia tweet zake za hivi karibuni ameongeza a.k.a ya ‘Anaconda’

Jide alijua kabisa kuwa inawezekana watu wakachukulia kama ni April fool’s day na kuchukulia tweet zake kama ni uongo, na hivyo alitoa tahadhari mapema sana kuwa tweet zake hazina uhusiano na April fool’s day na kila kitu ni ukweli, kwa maana hiyo hata radio yake ‘Kwanza FM’ ni kweli.

“Tatizo ni kuwa hata nikitweet vya ukweli mtachukulia ni April fool’s day, Mi nina Tweet vya ukweli ila nyie mtaamua sasa. Sizugi wala nini.” Alitweet Jide.

Lakini kwa kuwa watu wengi wanajua Jay Dee ametokea mkoa wa Mara walianza kuhisi kuwa labda atakuwa Mkurya kwa anaweza kuwa na asili ya hasira kama wengi wanavyoamini, na hapo Jide aliwafafanulia kwa tweet yake.

“Mimi sio mkurya ila nina joto hasira #JotoHasira”

Tunakutakia mafanikio mema zaidi tuongeze kituo kingine cha radio, na hiki kitakuwa cha kwanza kumilikiwa na msanii/mwanamuziki wa kike Tanzania.

0 comments:

Post a Comment