Blogger Widgets

Tuesday, April 16, 2013

Kumbe Wimbo mpya wa Diamond ‘Mapenzi basi’ umevuja! Awalaumu AM Records kwa kuvujisha nyimbo zake makusudi, anaweza asifanye nao kazi tena.

                           
Diamond platinumz kila akitoa wimbo hushika attention ya watu wengi na kuwa hit, lakini kumekuwa na mfululizo wa kesi za nyimbo zake kuvuja ikiwa ni pamoja na wimbo wake wa ‘Ukimwona’ na video ya wimbo wake ‘Kesho’.

theHOODinfotainmentimemtafuta Diamond Platinumz ambae alifunguka kuwa wimbo huo ulivuja. Aliwalaumu sana AM Records na kwa kile alichodai kuwa wanajua ni kwanini wao wameamua kuvuja wimbo huo japo wanakwepakwepa.

“AM record wenyewe sijui wanachonitafuta ni nini nikirekodi nyimbo kwao wanakuwa wanazivujisha yani makusudi. ” Alifunguka Diamond. Alisisitiza kuwa anajua AM Records ndio wako responsible kwa zoezi la kuvujisha nyimbo zake, “yani ni wao mi najua kabisa ni wao, wanaongea ila wanakuwa kama wanakwepakwepa ila mi najua kabisa ni wao.”

Huu sio wimbo wa kwanza kwa Diamond platinumz kuwa na matatizo kutoka AM Records, ‘Ukimwona’ pia ni wimbo ambao ulivuja na ulipikwa na AM Records, lakini Nataka kulewa iliyozua gumzo pia ilifanyika katika studio hiyo hiyo chini ya producer Maneck.

‘Kesho hit maker’ amesema baada ya wimbo wake ‘Ukimwona’ kupigwa sana japo hakuitoa officially na imeshahit basi ameamua kuacha ipigwe tu wakati anaangalia ngoma yake nyingine ya kuachia.
 
  theHOODinfotainment inaendelea kufanya jitihada za kumtafuta Manecky wa AM Records ili kujua kwa upande wake nini kinatokea hadi nyimbo za Diamond zinavuja kutoka katika studio hiyo.
 
chanzo: kwa msaada wa leotainment

0 comments:

Post a Comment