Blogger Widgets

Saturday, April 13, 2013

hii hapa ndio TOP 10 ya Rappers/waimbaji wa Bongo wenye mbwembe (swag) waongeapo kwenye redioni/TV

Uongeaji ni sanaa pia ambapo kuna wale waliojaaliwa uwezo wa kuongea kwa mbwembwe zaidi na kuwa kivutio kwa wanaosikiliza. Hawa ni wasanii 10 tunaoamini kuwa huongea kwa mbwembwe zaidi wahojiwapo redioni ama kwenye TV.

1. Godzilla
537094_510036565715287_1984810408_n
Kama haumfahamu Godzilla a.k.a Zizi na hujawahi kumsikia popote, ukifungulia redio na ukakuta anahojiwa unaweza kuhisi ni mnyamwezi fulani aliyekaa Marekani kwa muda mrefu sana na Kiswahili kimeanza kumtoka kichwani. Tangu aanze muziki, Zilla amekuwa akifuata nyendo nyingi za 50 Cent hasa katika kurap na kuongea. Mara nyingi kwenye interview hutupia swag kama za 50 na kwa hakika hakuna anayemfikia.

2. TID
16164_10151298061133749_1713734388_n
Khalid Mohamed aka Top in Dar huongea kwa kujiamini na dharau kiasi ndani yake (ndivyo alivyo). Katika interview hupenda kuchanganya Kiingereza mara kwa mara ambacho anakimudu poa pia. Mfano mzuri ni kwenye U Heard ya juzi kati ya XXL, Clouds FM kuhusiana na kukwaruzana kwake na Salama Jabir. Mwishoni mtangazaji wa show hiyo Soudy Brown alimuuliza TID anafanya nini maskani, na TID kujibu, “Nipo naangalia tambala moja hivi kwenye 3D kwahiyo I need a lot of attention, I am very sorry can you hang up for me!!”
3. Mr Blue
blue
Blue amepunguza tu mbwembwe siku hizi lakini kama ingekuwa enzi zile, Godzilla asingefua dafu. Blue ni tozi kitambo na ndiye mhasisi wa utamkaji wa maneno ya Kiswahili kwa ladha ya kimombo kwa mfano kabisa itamkwe, kabaisa kitu kilichofanya kuzaliwa kwa aka yake Kabayser.

4. Fid Q 543741_10151360853036641_1727557302_n
Fid aka Ngosha si mkali tu wa mashairi yenye swagga za moto bali pia hata uongeaji wake. Pamoja na kwamba anatokea Mwanza ambako Kiswahili cha huko kimeathiriwa na kisukuma, Fid huongea kama kashuka jana kutoka states. Uongeaji wake akiwa redioni utadhani ana kigugumizi fulani kumbe ndio swag ziko on. Izingatiwe pia kuwa The Top of Rap’s elite ni profesa wa Kitaalojia.
5. P-Funk
PFunk
Majani ni muongoezaji mzuri sana redioni. Background yake ya elimu na kutembea sehemu kadhaa duniani, kumemfanya asound kama Mmarekani aongeapo kimombo.

6. Shetta
482682_173480782804671_508310274_n
Shetta aka Bonge la Bwana naye yumo. Anapokuwa akiongea redioni huwa haoni hatari kutupia maneno kadhaa ya kimombo kushtua kidogo.

7. Q Chilla
IMG_5202-400x6002
Chilla ana uongeaji wa taratibu lakini wenye mbwembwe za hapa na pale hasa za kuchomekea viingereza.
8. Izzo B
fe4d86ff65b7b8263ce545dccb7a3ac0
Uvaaji wa Izzo na uongeaji wake vinaenda sawa. Izzo ni bling blinger na hewani anapokuwa anahojiwa, hit-maker huyo wa Riz-one hutupia swagga kibao na kama anahojiwa na mtangazaji mbovu si ajabu yeye ndio akasound kama mtangazaji wa show, ana vocal kali.

9. Quick Rocka
24290_3772466809924_1396166688_n
Quick aka Switcher kama anavyojiita, ni rapper anayeswitch swag kama kinyonga anavyobadili rangi yake. Kama Izzo B, yeye pia ana sauti ya mamlaka hewani.

10. Mo Rocka
Sijui nini kilitokea kwa rapper huyu mtanashati lakini kwa speed aliyokuja nayo kama angekaza, angekuwa mbali. Wakati anaanza kupata umaarufu wengi walikuwa wakimfananisha na Kabayser hasa kwa jinsi anavyorap na hata uongeaji wake kwenye redio.

0 comments:

Post a Comment