Blogger Widgets

Tuesday, September 10, 2013

KILI MUSIC TOUR 2013” KUHITIMISHWA JIJINI DAR JUMAMOSI


Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe akitilia msisitizo.

Msanii wa muziki wa bongoflava, Diamond akiwakaribisha watanzania kuhudhuria tamasha hilo. 
Msanii toka mwamba wa kaskazini, Joh Makini akieleza machache.
---
Na Kajunason Blog

Tamasha kubwa la “Kili Music Tour” lililoandaliwa na Tanzania Breweries Limited (TBL) chini ya nembo ya Kilimanjaro Premium Lager linahitimishwa na show kubwa ya Dar es Salaam Jumamosi hii tarehe 14 katika viwanja vya Leaders Club.

Ziara hii kubwa ya muziki mpaka sasa imefanyika kwenye mikoa 7 nchini kote ambapo zaidi ya wasaniii 28 wameshirikishwa ikijumuisha baadhi ya wateule na washindi wa mashindano ya Kili Tanzania Music Awards 2013 pamoja na wasanii wengine wanaong’ara kwenye fani ya muziki nchini.

Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Bwana George Kavishe alinukuliwa akisema kuwa ziara hizi ni sehemu ya juhudi za chapa ya Kilimanjaro Premium Lager katika suala zima la kuhamasisha na kuinua muziki wa Kitanzania, hususan, kwa wanamuziki wa nyumbani; vilevile ni tunu ya heshima kwa watanzania kwa kuendelea kuunga mkono
bia ya Kilimanjaro.

“Kili Music Tour 2013 ilizinduliwa na kauli-mbiu ya “Kikwetu Kwetu” ambayo ni kampeni ya Kilimanjaro Premium Lager ya kuhamasisha hisia za uzalendo kwa watanzania kwenye kuthamini vitu ambavyo ni vya kwetu na ni vyakitofauti kabisa kama lugha yetu ya Kiswanglish, muziki wetu wa bongo fleva, dansi yetu ya kiduku, kandanda yetu yenye upinzani wa Simba na Yanga, na bia yetu ya Kilimanjaro ambayo imetengenezwa Tanzania, na viungo vya kitanzania na watanzania kwa ajili ya Tanzania.” Alisema bwana Kavishe.

“Ziara ya mwaka huu ilikuwa ni kubwa kuliko zote zilizopita kwani tuliongeza mikoa na kufikia minane kutoka mitano ya mwaka jana na tuliongeza idadi ya washiriki wa tamasha kufikia zaidi ya 28. Vile vile tulishirikisha, si tu washindi wa 2013 wa ‘Kili Tanzania Music Awards’ pekee, bali pia na baadhi ya wateule wa tuzo na baadhi ya wanamuziki mashuhuri wanaong’ara katika tasnia ya muziki. 

Kwa kuwa Kilimanjaro Premium Lager ni bia ya kizawa iliyoasisiwa Tanzania inatambua ni kwa kiasi gani watu wetu wanajivunia upekee wa kitanzania kama ilivyo bia yao hii na ndiyo sababu kubwa iliyotufanya tuwapeleke wanamuziki walio bora katika fani kwenye milango ya washabiki huko waliko mikoani kupitia mtindo wetu wa ‘Kikwetu kwetu!” alimalizia bwana Kavishe.

Wasanii 14 watashiriki watashiriki kwenye tamasha la Dar es Salaam ambao ni:- Diamond Platinum, Professor J, Ben Pol, Lady Jay Dee, Lynex, Roma, Recho, Kala Jeremiah, Joh Makini, Mzee Yusuph, Mashujaa Band, Ney wa Mitego, Ras Six na
Tip Top Connection.NA LUKAZA BLOG

0 comments:

Post a Comment