Blogger Widgets

Thursday, September 5, 2013

MNIGERIA ANASWA NA KETE 99 ZA MADAWA YA KULEVYA JNIA


 
Anthonia Ojo (25) akitoa madawa ya kulevya katika makopo ya poda na shampoo baada ya kukamatwa.
Mzigo aliodakwa nao Anthonia Ojo huu hapa.
Mtuhumiwa huyu hapa.
Begi alipokuwa ameweka mzigo huo.
-ALIKUWA AKIELEKEA ITALIA KUPITIA UFARANSA
-ALIYAFICHA KATIKA MAKOPO YA PODA NA SHAMPOO

-ADAI KUYANUNUA MAGOMENI

-UCHUNGUZI UKIBAINIKA ATAPANDISHWA KIZIMBANI

Mwanamke Anthonia Ojo (25), raia wa Nigeria akiwa na kete 99 za madawa ya kulevya amekamatwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam jana, akieleke Roma, Italia kupitia Paris, Ufaransa kwa ndege ya Ethiopian Airways. 

Mwanamke huyo aliingia hapa nchini Agosti 30 akitokea nchini Nigeria na baada ya kuhojiwa alidai kuwa dawa hizo alizinunua maeneo ya Magomeni, jijini Dar es Salaam. 

Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Viwanja vya Ndege, Renatus Chalya, Ojo anaendelea kubaki chini ya ulinzi wa polisi kwa uchunguzi zaidi, wakati madawa hayo yakipelekwa kwa ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali ili kubaini aina ya dawa hizo, thamani yake na hatimaye atafikishwa mahakamani.
Passport ya Ojo.
...Ojo akishushwa kwenye gari baada ya kukamatwa.
...Mikononi mwa polisi.
Madawa aliyonaswa nayo Ojo baada ya kutolewa kwenye makopo.
Credit: Robert Okanda

0 comments:

Post a Comment