Blogger Widgets

Monday, September 16, 2013

MR.NICE KATIKA MZOZO MWINGINE!

nice
Nguli wa muziki aina ya ‘Takeu’ Lucas Mkenda ameingia katika mzozo mzito na meneja wake mpya baada ya kutokukubaliana baadhi ya mambo aliyokuwa akishauriwa na lebo hiyo mpya.
Mr Nice ambaye kwa sasa anamilikiwa na lebo ya Candy&Candy Records  kwa muda wa mwezi mmoja na nusu sasa baada ya kutoka katika familia kubwa ya muziki ya GrandPa Recods, ameelezwa kuwa alikuwa na mtazamo tofauti kibiashara na kampuni hiyo hali iliyotishia kuvunjwa kwa mkataba wao.
Akizungumza na gazeti hili jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Kampuni ya Candy&Candy Records, Joe Kariuki alisema kampuni na mwanamuziki huyo anayependwa nchini Kenya ilitokea kutofautiana katika baadhi ya mambo hasa ubora wa kazi.
“Mr Nice ni msanii anayependwa sana hasa Mombasa, lakini wiki chache zilizopita tulikuwa na mabishano kidogo hii ilitokana na mtazamo tofauti hasa ni kutokana na wimbo wake mpya wa ‘Akina Mama’ binafsi ule wimbo sikuupenda na nilimshauri kwamba ni vyema tungetumia wimbo mwingine, lakini aling’ang’ania
 

0 comments:

Post a Comment