Blogger Widgets

Monday, September 30, 2013

WEMA AENDA KUFANYIA BETHIDEI CHINA!

Wema Isaac Sepetu (kulia) akipozi na Aunty Ezekiel wakati wa pati ya ‘bethidei’ yake.
Na Imelda Mtema

JEURI ya Fedha! Wema Isaac Sepetu a.k.a Madam ameenda Hong Kong nchini China na kufanyia huko bonge la pati ya ‘bethidei’ yake wakati akitimiza umri wa miaka 25 huku staa mwenzake, Aunty Ezekiel akiungana naye akitokea Dubai.…

Wema Isaac Sepetu (kulia) akipozi na Aunty Ezekiel wakati wa pati ya ‘bethidei’ yake.
Na Imelda Mtema
JEURI ya Fedha! Wema Isaac Sepetu a.k.a Madam ameenda Hong Kong nchini China na kufanyia huko bonge la pati ya ‘bethidei’ yake wakati akitimiza umri wa miaka 25 huku staa mwenzake, Aunty Ezekiel akiungana naye akitokea Dubai.

...Madam ndani ya Hong Kong.
Habari kutoka Hong Kong zilisema kuwa Madam alifanya tukio hilo Ijumaa iliyopita Septemba 27, mwaka huu ambapo aliongozana na ndugu yake aliyetajwa kwa jina moja la Bite huku Aunt akiungana naye akitokea kwa mumewe, Sunday Demont huko Dubai.
Ijumaa Wikienda lilipenyezewa picha za tukio zikiwaonesha Wema, Aunt na ‘kampani’ zao wakipiga vinywaji vikali na bata nyingine za kufa mtu.

...Madam 'akishow' love.
Tukio hilo lilisababisha Wema kupokea hongera nyingi kutoka kwa mastaa wenzake, mashabiki na watu wa kawaida akisifiwa kuwa amewaziba midomo wasanii wenzake kwa kwenda kusherehekea siku yake ya kuzaliwa Hong Kong.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda kutoka Hong Kong, Aunt alisema kuwa alikwenda Dubai kwa mumewe lakini alikuwa na taarifa kuhusu pati ya Wema hivyo alivyofika Dubai alianza taratibu za safari za kuelekea Hong Kong.

0 comments:

Post a Comment