Mmomonyoko wa maadili katika vyuo vikuu
hapa nchini umekuwa ukisababishwa na ugumu wa maisha na kucheleweshwa
kwa hela ya kujikimu toka bodi ya mikopo ya elimu ya juu hapa nchni na
uongozi mbovu wa vyuo........
Wakiongea kwa nyakati tofauti na mtandao
huu, baadhi ya wanafunzi hao toka vyuo mbalimbali wamedai kuwa maisha
ya chuo ni magumu sana hasa kwa mtoto wa kike ambaye anahitaji vitu
vingi ili aweze kujikimu kimaisha.......
"Kwa kweli maisha ya chuo ni magumu
sana hasa kwetu sisi wasichana.Hela yetu ya kujikimu huchelewa
sana.Wazazi nyumbani wanajua kuwa tuna mkopo na wengine wanaimani finyu
kuwa tunalipwa na serikali.......
Ukiomba hela
nyumbani unagombezwa na hupewi au wakikuonea huruma watakurushia
30,000 .Sasa hiyo hela inatosha kula, kununua mafuta,kusuka na vitu
vingine?".......
Katika hali kama
hii, inakuwa ni vigumu sana kwa mtoto wa kike kuvishinda
vishawishi......Na ndipo tunapolazima kutafuta sehemu ya kujihifadhi
kwa wakaka......" Alieleza binti mmoja ambaye hivi sasa ni mwaka wa pili ( chuo tunakihifadhi)
Mbali na maoni hayo, mwanafunzi mwingine toka ukanda wa pwani alikuwa na mtazamo tofauti:
"Tatizo ni malezi ya kila mtu. Chuo na mapenzi havina uhusiano wowote.Mbona hata hata huko mtaani mapenzi yapo? Kwa nini wasilaumiwe wao? Suala la msingi ni kwamba siku hizi uzushi mwingi.
Wanaume wanatembea na simu zenye kamera. Ukilala anakupiga picha alafu mkiachana anakuweka facebook."
Maoni ya huyu binti yalimfanya mwandishi
wetu atake kujua zaidi juu ya asili ya picha hizo za utupu maana
zimekuwa zikipigwa katika pozi na si kwa kuviziwa....
"Ni kweli baadhi yetu hufanya hivyo.Sasa hayo nimakubaliano yao.Pengine kaambiwa kwa kufanya hivyo atapewa hela ndefu zaidi na ukizingatia mfukoni hana kitu na boom halitabiliki.Unadhani atafanyaje? .....
Kwa asilimia kubwa wasichana tupo katika wakati mgumu sana.Hata sisi hatupendi kupigwa tukiwa uchi ila tunalazimika kutokana na mazingira"
CHANZO; MPEKUZI