Blogger Widgets

Monday, March 11, 2013

JUSTIN TIMBERLAKE AJIBU DISS YA KANYE WEST


Wiki mbili zilizopita the big boss wa kampuni ya good music mkali yeezy.. kanye west alikaririwa na vyombo mbalimbali vya habari akisema kuwa yeye anamzimia hov/jay z, lakini sio jigga man wa “suit & tie” akimaanisha ngoma ambayo jay – z alikua chini ya kiwango. Ngoma hiyo ni ngoma aliyoshirikishwa na Justine Timberlake 


Baada ya diss ile ama changamoto, justin timber lake ameonyesha kuwa ile kauli ya kanye ilimuumiza na uzalendo ukamshinda akajikuta ana tiririka kupitia saturday night live show, katika ya performance ya wimbo huo “suit & tie".
 
Timber lake alipofika katika verse ya pili ya wimbo huo, alishangaza watu pale alipobadilisha mstari unaosema 

 “And aww, sh** so sick, got a hit and picked up a habit” na kusema 

“My hits so sick got rappers acting dramatic”


akiisifia ngoma yake kuwa ni kali mpaka inawafanya rappers waropoke vitu vya kijinga, hali ambayo inatafsiriwa kuwa ni dongo kwa kanye west.


jay z bado hajaskika akijibu chochote, tusubiri coz kuna tour inakuja this summer ni kati ya timber lake na jay z

0 comments:

Post a Comment