Katika
kuizunguka dunia nashukuru nimetembelea nchi nyingi duniani ikiwa
barani Afrika na kwengineko ambako nimejaaliwa kutembelea.
Nimekuwa najifunza kila kukicha jinsi watu wanavyoishi na mazingira kwa ujumla.
Nimekuwa najifunza kila kukicha jinsi watu wanavyoishi na mazingira kwa ujumla.
Kati
ya nchi saba za Afrika nilizobahatika kutembelea moja ya nchi ambazo
naweza kusema watoto wadogo walio na chini ya miaka 16 wamekuwa
wakijihusishaa na masuala ya vilevi kama Pombe,Bangi na madawa ya kisasa
ya kilevi `Drugs` ni nchi ya South Africa.South Afrika ni moja ya nchi
ambazo zimepiga hatua kimaendeleo kati ya nchi nyingine za
Afrika.Tatizo linakuja pale wenzetu wanavyoutumia uhuru wa malezi
vibaya.
Nikizungumzia
malezi nazungumzia makuzi ya watoto na wazazi wao.Ndugu zetu wa South
Afrika wametoa uhuru kwa watoto wao vibaya sana tofauti na mila na
tamaduni za makabila au nchi nyinginezo barani Afrika.
Nchini South Africa kumuona mtoto wa kike anavuta bangi ni jambo la kawaida,kuwaona wanafunzi wakiwa na pombe ni kitu cha kawaida tofauti na kwengineko barani Afrika.
Nchini South Africa kumuona mtoto wa kike anavuta bangi ni jambo la kawaida,kuwaona wanafunzi wakiwa na pombe ni kitu cha kawaida tofauti na kwengineko barani Afrika.
Suala zima la uhuru kwa watoto lisipotiliwa mkazo na kipaumbele
tutakosa wataalamu wazuri duniani,totakosa taifa bora lenye upeo mzuri
kimaendeleo,na hii sio tu kwa South Afrika bali na kwengineko duniani.
Malezi bora kwa watoto ni jukumu la mzazi na mtu yoyote mwenye kuelewa umuhimu wa ulezi.
Nasema hivi nikiwa na maana nyingi ila mojawapo ni kwamba anapoathirika mtoto wa mwenzio kumbuka hata wewe athari hizo zitakuathiri na wewe kwa njia nyinginezo.

Picha
ya juu ukiangalia vyema utaona jinsi gani wanafunzi walivyoshiriki
katika suala la ulevi na kinachofuata hapo ni ngono zembe,kubakwa pasipo
kutarajia,maambukizi ya ukimwi na magonjwa mengineyo ya zinaa.
Mwanafunzi mlevi kwa asilimia kubwa hana muelekeo mzuri katika masomo
yake.Wazazi chonde chonde tuwaangalie watoto wetu ili kulinusuru Taifa
letuss
0 comments:
Post a Comment