Janet.
NINI
tafsiri ya uelekeo wa dunia kutokana na matukio ya kutisha? Upo ukatili
mkubwa umefanyika nchini Nigeria ambapo mume amemwagia mkewe mafuta ya
petroli na kumchoma moto.
Kehinde
Adesamuye, 39, mkazi wa Lagos, Nigeria anadaiwa kumchoma kwa moto wa
petroli hivi karibuni mkewe Janet Udegba, 35, katika Mtaa wa Ikotun
jijini Lagos baada ya kuwa na hasira kutokana na kuhisi kuwa ana
uhusiano wa kimapenzi na mwanamume mwingine.
Janet
alisema wakati wa tukio hilo, alikuwa katika eneo lake la biashara
akiuza vyakula kabla ya Kehinde kufika hapo usiku huo na kumwagia
petroli mgongoni kisha kuwasha moto kwa kutumia kibiriti.
Hata hivyo, alisema Wanigeria hawatamwachia huru Kehinde kutokana na kile alichokifanya. Akisimulia mgogoro wao, anasema:
“Mume wangu amekuwa na wivu daima.
Amekuwa na tabia ya kunipiga kila wakati. Nimejaribu mara nyingi
kuachana naye lakini huwa ananitishia kuwa lazima atanidhuru.
Niliendelea kuishi naye kwa kuwa nilikuwa na hofu ya maisha yangu,
aliwahi kuniambia kuwa sitaweza kutoroka hata siku moja.
“Serikali lazima ihakikishe kuwa Kehinde
analipa kwa kile alichonifanyia. Mimi ni yatima, ninafanya biashara ya
vyakula ili niishi. Sasa nimetumia pesa zangu zote kwa ajili ya
matibabu. Kwa kweli kwa sasa nahitaji msaada,” alisema mama huyo huku
akitokwa machozi.
Kehinde alijaribu kutuma rafiki zake ili
wamwombee msamaha kwa Janet lakini alikataa. Mtuhumiwa huyo
anashikiliwa na polisi kwa ajili ya kujibu mashtaka yanayomkabili.
Global Publishers
0 comments:
Post a Comment