Kwa ufupi
MSANII anayeaminika kuwa na nyota ya kupendwa na
mashabiki na wadau wengi wa muziki wa kizazi kipya hasa wanawake, Naseeb
Abdul au Diamond Platinumz kama anavyojiita, amejitokeza kujibu tuhuma
kadhaa zinazomkabili.
MSANII anayeaminika kuwa na nyota ya
kupendwa na mashabiki na wadau wengi wa muziki wa kizazi kipya hasa
wanawake, Naseeb Abdul au Diamond Platinumz kama anavyojiita,
amejitokeza kujibu tuhuma kadhaa zinazomkabili.
Hatua hiyo imekuja baada ya maswali mengi kuibuka
na shutuma nyingi kumwangukia kupitia vyombo mbalimbali vya habari, huku
akiwa amekaa kimya, kiasi cha kufanya baadhi ya watu kutoelewa ni kwa
nini ameamua kutozungumza chochote.
Moja ya tuhuma kubwa inayomkabili ni kuhusiana na
mganga wa kienyeji anayehangaika kwenye vyombo vya habari na kudai
kwamba amemfikisha Diamond hapo alipo lakini kwa sasa amekimbiwa na
msanii huyo.
Akijibu tuhuma hiyo akasema kwamba kwanza hamjui
huyo mganga, ila kiukweli ni kwamba kuna watu wanataka kumchafua, na
kama ni mganga kweli na kakimbiwa na mteja aliyempandisha kwa nini
asitumie uganga kumshusha?
"Mganga wa kweli jamani hawezi kukimbilia kwenye
vyombo vya habari, mganga wa kweli anamalizana na mteja kimya kimya na
mteja mwenyewe anajikuta anarudi kwa mganga kuomba radhi, huyu sio
mganga, ingawa simjui!”
Tuhuma ya pili ni kuhusiana na maonyesho yake
kudorora ambapo pia mganga huyo amehusishwa, kwamba yeye ndiye
aliyemlaani na kusababisha mambo ya mwanamuziki huyo anayefikiriwa kuwa
ni tajiri kuliko wenzake, kuanza kwenda mrama.
Jibu alilolitoa ni kwamba hakuna jambo lake hata
moja linalokwenda vibaya. Picha zilizochapishwa na gazeti moja la kila
wiki, likionyesha ukumbi ukiwa mtupu katika onyesho ambalo alilifanya
Arusha, zilipigwa mwanzoni, wakati hapakuwa na mashabiki wengi waliokuwa
wameingia, ukumbi baadaye ulijaa.
"Na kama ni maonyesho, nina ratiba ya show mpaka
mwezi wa saba, sasa nimeshuka vipi jamani?", alisema huku akionekana
mwenye masikitiko makubwa kwa kile anachosema anaonewa tu na maneno hayo
ya uzushi.
Habari nyingine kubwa iliyoenea mjini ni ile
inayohusiana na uhusiano wake na Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya
Entertainment Masters, Peniel Mungilwa ambapo katika mitandao ya kijamii
wamekuwa wakionekana mara kwa mara wakiweka picha zao zinazoonyesha
dhahiri wapo katika mapenzi.
Hili alionekana kama kushtushwa nalo ingawa
baadaye alijiweka sawa na kusema ni sinema tu za hapa na pale lakini si
ukweli kwamba wana uhusiano.
0 comments:
Post a Comment