Msanii H baba leo hii amefunguka kupitia 255 ya xxl, kuwa hakuna msanii
hata mmoja ambae ameweza kufanya show nyingi kama yeye kwa mwaka 2012,
na kuwa, alifanya show 625 ndani ya mwaka huo..
"kama unajua mwakajana nimevunja rekodi ya show, hakuna msanii amepiga
show nyingi kama mimi, mi nimepiga show 625, hakuna msanii kafikia
rekodi yangu mimi yoyote, 625 show nilizopiga mwaka jana. mpaka sasa
hivi kwa mwaka huu, nimefungua na koffi, nyuma nilikuwa na mikataba ya
safari lager, sijui tigo, sijui nini, show zangu mwenyewe, show ni
nyingi, 625 show nilizofanya mimi mwaka jana.kuna sengerema, magu,
wapi, mi huwa nahesabu tu show zangu, mikataba niliyofanya show 50 sijui
100 zote mi nafanya, hizo ni kazi zangu mie.nilikua na perform ijuma
jumamosi na jumapili.."
"unajua sisi wasanii tunakula kilaini sana tuseme, tofauti na
wafanyakazi wa serikalini anasubiri mshahara mwisho wa mwezi ushaelewa?
hasa lazima nijitume kwasababu ni hela ambayo naipata kwa masaa mawili,
kwa hiyo siwezi kusema najiskia uchovu sana siwezi kufanya kazi zingine
huo ni unafki, kuna mtu anafanya kazi analipwa laki nne tu au laki mbili
na anaenda kazini kila siku na anatumia nauli yake kwenda, mi nalipwa
show milioni 2, milioni 3 nna wasiwasi gani, mwaka huu mpaka sasa hivi
nina show 8, ndio nimeanza nina show 8." amesema H baba
0 comments:
Post a Comment