Ikiwa ni miezi mitatu tu
imepita toka nchi nyingine ambayo ni maarufu Afrika (Kenya) kukumbwa na
headlines za kutosha kuhusu raia wake wanaoshiriki mapenzi ya jinsia
moja kupeana tuzo hadharani na kufanya sherehe, leo tena headlines
zimehamia Nigeria.
Ndani ya miaka mitano iliyopita
huko Nigeria kulikua na Kanisa ambalo lina waumini wanaoshiriki mapenzi
ya jinsia moja tu liitwalo House of Rainbow lakini Kanisa hilo
lilipotea baada ya kushambuliwa na wakazi wa Lagos ambao hawapendezwi na
ishu za ushoga na usagaji.
Tarehe 3 March 2013 Mtandao
maarufu wa Nigeria wa TFJ umeripoti kwamba kanisa hilo limerejea tena
kwa kishindo na kuendelea na huduma zake.
Ni kanisa ambalo mwanzilishi
wake ni mchungaji Mnigeria ambae ni shoga Rowland Jide Macaulay na
imefahamika sasa hivi kwamba kanisa hilo lipo Ghana na Malawi, France,
Netherlands, Cote d’Ivoire na Sierra-Leone.
0 comments:
Post a Comment