Blogger Widgets

Tuesday, June 11, 2013

ALICHOKISEMA SEBO WA MAGIC FM KUHUSU BEEF YA RUGE NA JAYDEE "KAMA NINGEKUWA RUGE NINGEMPIGIA MAGOTI LADY JAYDEE NA KUMUOMBA MSAMAHA"

Katika kipindi cha Sun Downer cha Magic FM, mtangazaji huyo amesema kwamba shangwe zilizolipuka mara baada ya Jaydee kutajwa kuwa miongoni mwa wanaowania tuzo ya msanii bora wa kike katika tuzo za KTMA, ni ishara ya mwanadada huyo kukubalika katika jamii. 

Mtangazaji huyo amesema kwamba Jaydee ni mwanamke mwenye uthubutu katika harakati za kuyasaka maisha na kwamba yeyote mwenye nia ya kukwamisha jitihada zake aibu na iwe juu yake. 

Ameongeza kuwa kukubalika kwa mwanadada huyu pia kulidhihirika pale watazamaji katika tukio hilo walipomshinikiza 

Meneja wa msanii huyo (Gadna) kutaja kiingilio na tarehe ya maadhimisho ya miaka 13 ya Jaydee katika uga wa muziki. Hivyo, Sebo anaona ni vyema Ruge akajishusha na kumaliza tofauti zake dhidi ya Jaydee.


0 comments:

Post a Comment