Blogger Widgets

Wednesday, June 12, 2013

UKUMBUSHO: TAREHE KAMA YA LEO, RAIS NELSON MANDELA ALIFUNGWA MIAKA 27 JELA?

Siku kama ya leo (June 12) mwaka 1964 viongozi wapatao 8 wa chama cha ANC akiwemo rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela walihukumiwa kwenda jela, ambako mzee Mandela alitumikia kifungo kwa miaka 27.

Mzee Madiba ambaye leo anafikisha siku ya 5 akiwa amelazwa hospitalini akisumbuliwa na mapafu huko Afrika Kusini, ndiye alikuwa rais wa kwanza mweusi kwa taifa hilo.


Kwa mujibu wa BBC Kwa sasa Afya ya Mandela bado si nzuri na Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini anaendelea kuwaomba wananchi wa taifa hilo kuendelea kumuombea mzee Madiba aweze kupona.

1 comment:

  1. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete