Blogger Widgets

Wednesday, June 5, 2013

HIKI NDO KILICHOTOKEA HADI DIAMOND KUTAKA KUSABABISHA TARATIBU ZA KUAGA MWILI WA MANGWAIR KUTAKA KUVURUGIKA


MSANII maarufu wa muziki wa kiazazi kipya nchini Tanzania Abdul Nassib (Diamond Paltinumz) alifika katika viwanja wa Leaders Club na  kupata nafasi ya kutoa heshma ya mwisho kwenye jeneza la aliyekuwa msanii mwenzake wa muziki wa kizazi kipya Albert Mangwea.


Mangwea ambaye alifariki Dunia katika Jiji la Johannesburg nchini Afrika Kusini Mei 28 mwaka huu, mwili wake uliwasili nchini Tanzania  jana na kupokelewa na maelfu ya mashabiki wa muziki wake na hatimaye mwili kupelekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kuhifadhiwa.

Mwandishi wa habarimpya.com aliyekuwa katika viwanja hivyo alimshuhudia Diamond pamoja na baadhi ya wasanii wenzake  wakiuungana na maelfu ya watanzania waliofika katika viwanja  hivyo.

Akiwa amevalia nguo za rangi nyeusi kama ilivyo kawaida ya watu wanaojua kubangilia mavazi kulingana na matukio huku wengine pia wakitupia kitu cha rangi nyeupe,hata hivyo msanii huyo kipenzi cha mashabiki wa muziki wa kizazi kipya hususan wakina dada kutoka nyimbo zake za kulilia mahaba ya warembo alijikuta akiharibu utaratibu mzima wa kuuaga mwili wa Mangwea.

Ingawa Kamati ya mazishi ilishatangaza kufunga zoezi la kuuaga mwili huo, Diamond aliinuka kwenye kiti chake kwa lengo la kuondoka uwanjani hapo, ghafla alivamiwa na mashabi wa muziki wake waliokuwa wakihitaji kuongea naye. Tukio hilo lilisababisha umati wote uliokuwa wakisubiri msafara wa mwili wa Mangwea kuondoke uwanjani hapo kutawanyika na kumkimbilia Platinumz hadi kweneye gari lake ambapo aliingia na bado wakaendelea kulifukuzia gari lake likiondoka viwanjani hapo.

0 comments:

Post a Comment