Blogger Widgets

Thursday, June 20, 2013

BAADA YA MSANII SAJNA KU-COPY IDEA YA "muziki gani" MSIKILIZE NEY WA MITEGO ALICHOKISEMA HAPA

 



Hivi karibuni msanii Sajna ametoa wimbo mpya unaokwenda kwa jina la MPIRA GANI ambayo ameshirikiana na msanii mwingine ajulikanae kwa jina la FREGE, kama umepata bahati ya kuusikia wimbo huo hauna tofauti kabisa na ule wa wasanii wakali bongo hapa niki mkusudia Ney wa mitego na Diamond ambao walishirikiana katika ngoma yao ya HUU NI MZIKI GANI, nisikuchoshe hebu tumsikilize mwenyewe Ney wa Mitego analizungumziaje suala hili la dogo kucopy idea yao.
Baada ya tukio hilo je Sajna yeye mwenyewe anasemaje kwanini aliamua kufanya hivi tena bila ya kuwahusisha wenye ngoma yao na mwisho wa siku ngoma ikawa hewani. Hebu tumsikilize naye anasemaje.
Hizo ndizo kauli zao ndugu, nawapongeza sana hasa Ney wa Mitego kwa Uamuzi wake wakujua kuwa Dogo ni mmoja wa Mashabiki wake na Kwa upande mwingine naye ni Msanii ambaye anatafuta namna ya kutoka hivyo jambo zuri ni ushirikiano katika Inderstry hii ya Mziki.. BIG UP SANA MKUBWA NEY WA MITEGO



0 comments:

Post a Comment