Blogger Widgets

Friday, June 28, 2013

KAJALA ATAKIWA KUACHA UNAFKI

   

Na Mwandishi Wetu
BAADHI ya wasanii wa filamu Bongo wamemtaka mwenzao, Kajala Masanja (pichani) kuwa mkweli kuhusiana na ushosti wake na Wema Sepetu kwani kudai kwamba wako sawa wakati ukweli unajulikana ni unafiki.
Wakizungumza na Ijumaa juzikati, baadhi ya wasanii hao walioomba majina yao yasiandikwe gazetini walisema wameshangazwa na maneno ya Kajala kwenye mtandao kuwa hana tatizo na Wema wakati wao wanajua wametofautiana.

“Mlipoandika kuwa Wema na Kajala wametibuana sikushangaa kwani ndiyo ukweli lakini nikaona kwenye mtandao Kajala anasema eti yuko sawa na Wema, aache unafiki, awe mkweli tumsaidie maana sisi tunamjua vizuri Wema. Ili uwe rafiki yake ufunge mkanda,” alisema mmoja wa wasanii hao ambaye pia ni rafiki wa karibu wa Kajala. NA GPL

0 comments:

Post a Comment