Blogger Widgets

Tuesday, June 18, 2013

Kaka wa marehemu Langa, Maurice Kileo asema mdogo wake alikuwa kiungo kikubwa katika familia yao

MAURICE KILEO
Maurice Kileo


Kaka mkubwa wa msanii Langa Kileo aliyefariki dunia wiki iliyopita na kuzikwa jana kwenye makaburi ya Kinondoni jijini Dar, Maurice Kileo amesema marehemu Langa alikuwa kiungo muhimu wa mawasiliano kwenye familia yao. Akizungumza kupitia Clouds E ya Clouds TV, Maurice alisema Langa alikuwa kijana aliyependa kujifunza.

“Langa tangu anakua alikuwa mtu ambaye anapenda kujua vitumbalimbali kwenye fani tofauti,”alisema Maurice.

“Tangu mtoto ni mtu anayependa kujifunza vitu tofauti na pia alikuwa kiungo katika familia kwa kuwa mtu anayependa kuwasiliana na watu wote wa familia yetu. Sisi tuna ndugu zetu kwenye familia wanaoishi nje ya nchi na wengine tupo hapa, yeye mwenyewe ndiyo alikuwa anawasiliana na watu wote hawa vizuri tu,”aliongeza.

“So, naweza kusema kama tumempoteza mtu ambaye alikuwa ni kiungo katika familia.”

Unaweza kuangalia Clouds E kupitia Clouds TV kila siku saa mbili usiku na marudio kesho yake saa nne asubuhi na saa sita mchana.

0 comments:

Post a Comment