Blogger Widgets

Sunday, June 16, 2013

WAKENYA WAMLILIA LANGA .... NI KWANINI WANAMLILIA ZAIDI BAADA YA KIFO CHAKE? .... RIPOTI KAMILI HII HAPA

WADAU wa muziki nchini Kenya wameguswa na kifo cha msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzanian Langa Kileo, kilichotokea jana jioni katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam.

Langa ambaye alikimbizwa katika Hostali hiyo siku tatu zilizopita aliwahi kutamba na kibao chake cha kwanza katika tasnia ya muziki iliyojulikana kwa jina la 'Langa matawi ya juu', kifo chake kimekuwa gumzo katika mitaa mbalimbali ya jiji la Nairobi.

 
Mwandishi Wetu akiripoti kutoka jijini Nairobi nchini Kenya anasema kwamba wadau wa muziki wamepokea kifo cha msanii huyo kwa hisia tofauti.

Jane Kimboi anasema kwamba alimfahamu Langa miaka mingi iliyopita wakati akiwa katika kundi la (Wakilisha) iliyokuwa ikiongozwa na Sarah Kaisi,ambapo baadaye waliweza kunyakuwa tuzo ya Coca Cola Popstars mwaka 2004.

"Hata hivyokundi la Wakilsha ilisambaratika mwaka mmoja baadaye, kama ilivyo kwa wasanii mbalimbali Duniani Langa alipoteza ndoto zake za kuwa msanii mkubwa ndani na nje ya Tanzania baada kujiingiza katika matumizi ya dawa za kulevya"anasema Kimboi.


Joseph Omolo anasema kwamba kifo cha Langa kimemwachia kumbukumbu ambayo hawezi kuisahau, ingawa marehemu hakuweza kutimiza ndoto zake kutokana na matumizi ya dawa za kulevya.

"Langa ni msanii pekee Afrika Mashariki aliyefanikiwa kupiga hatua kubwa baada ya kufanya maamuzi ya kuacha kutumia dawa za kulevya, Langa aliweza kufungua taasisi yake ya kuelimisha vijana juu ya matumizi ya dawa za kulevya"alisema Omolo.

Alisema kwamba Langa aliweza kufungua taasisi hiyo iliyoitwa 'Second Chance for African Addicts', na hata akafanikiwa kuachia wimbo wake uliofahamika kwa jina la 'Kifo' wimbo huo ulikuwa na maudhui ya kuelemisha jamii kuhusu madhara ya dawa za kulevya.

Omolo ambaye pia amewai kuwa mwathirika wa dawa za kulevya alifafanua kwamba, Hata hivyo Langa alikuwa na mipango ya kujenga kituo cha kulea na kusaidia vijana walioathiriwa na dawa za kulevya, ambapo angeweka watalaamu wa ushauri nasaha na saikalojia pamoja na vifaa vya mazoezi

Read more:
http://talkbongo.blogspot.com/2013/06/wakenya-wamlilia-marehemu-langa.html#ixzz2WJlsN3aL

0 comments:

Post a Comment