Blogger Widgets

Tuesday, June 18, 2013

Update: Habari za kufariki Saida Karoli zakanushwa


saida-karoli

UPDATE: Taarifa mpya zinasema ajali ya boti imetokea lakini Saida Karoli hakuwemo kwenye boti hiyo na yuko hai. Kwa taarifa hizo za kukanusha kufariki msanii huyo, nenda kwenye link ifuatayo: Taarifa: Saida Karoli yuko hai. Kweli ajali ya boti imetokea lakini Saida hakuwemo
Kwa mujibu wa Mjengwa blog mwanamuziki mashuhuri Afrika Mashariki, Saida Karoli amefariki dunia baada ya kuzama maji kufuatia ajali ya boti iliyotokea kwenye ziwa Victoria. Ajali hiyo ilitokea baada ya boti aliyokuwa akisafiria kutoka Kisiwa cha Goziba kukumbwa na dhoruba na kuzama katika Ziwa Victoria.
Taarifa hizo zinasema pamoja na Saida Karoli, kuna watu wengine pia wamefariki dunia katika ajali hiyo. Idadi ya waliofariki kwenye ajali hiyo bado haijapatikana

0 comments:

Post a Comment