Blogger Widgets

Monday, July 22, 2013

embu oneni jinsi Jay Z na Beyonce walivyoungana na mama mzazi wa Trayvon Martin katika maandamano yaliyofanyika jumamosi


 Maelfu ya wananchi walikusanyika katika miji zaidi ya 100 marekani siku ya Jumamosi 
(July 20) kupinga "Stand Your Ground Law" katika kumsapoti  Trayvon Martin, kijana mweusi mwenye miaka 17, ambae alipigwa risasi na kuuwawa na George Zimmerman 2012.

hiphop most famous  couples, Jay Z na Beyonce pia waliungana na wananchi hao.
Jay na Beyonce walihudhuria uhasamishaji huo wakiwa Manhattan, New York wakiongozana na Al Sharpton (Baptist Minister, Civil Rights/social justice activist, Radio and Tv talk show host)  na mama mzazi wa kijana alieuwawa  Sybrina Fulton.
"Jay-Z na Beyonce wamesema, hawakutaka kuongea, hawakuja kwa ajili ya kuonekana kwenye picha" amesema Al Sharpton, "Jay Z ameniambia mimi ni baba. Beyonce ni mama. Wote tunahisi uchungu na wasiwasi- sheria lazima zimlinde kila mtu, au isimlide yoyote, hatujaja kwa ajili ya chuki, tumekuja kwa ajili ya mapenzi na watoto"
Zimmerman alikutwa hana hatia ya mauaji ya shahada ya pili au bila kukusudia baada ya kesi hiyo kuendeshwa na kuonyeshwa live kupitia television ya taifa.
baada ya uamuzi kutangazwa kuwa Zimmerman hana hatia, emcees kama vile Technique Immortal, Brother Ali, Young Jeezy, na SpaceGhostPurrp, miongoni mwa wengine wengi, haraka walipingana na na  habari.

0 comments:

Post a Comment