Blogger Widgets

Tuesday, July 30, 2013

Mfahamu Director wa Video aliyehukumiwa kifungo cha miaka 90 gerezani kwa kuwabaka watoto wake

aswad 
Director wa Video Aswad Ayinde amehukumiwa kifungo cha miaka 90 gerezani kwa kosa la kuwabaka watoto wake mwenyewe na kuwazalisha watoto katika kipindi cha zaidi ya miaka 20 iliyopita .
Aswad mwenye umri wa miaka 55 alipewa hukumu hiyo hapo jana huko Marekani baada ya mahakama kumkuta na hatia ya makosa ya ubakaji na unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto wake mwenyewe.
Aswad alikuwa na tabia ya kuwabaka watoto wake ambapo aliwazalisha watoto kadhaa huku mwenyewe akisema kuwa alifanya hivyo ili kuweka damu yake karibu .

Mke wa Aswad ambaye alikuwa mmoja wa watu waliotoa ushahidi dhidi ya director huyo Beverly Ayinde amesema kuwa baba yao aliwalazimisha mabinti zake kufanya nao mapenzi na kuwazalisha watoto ambao alihakikisha wanazaliwa chini ya uangalizi wake na hawakuruhusiwa kusoma shule za kawaida ambapo walifundishiwa nyumbani.
Beverly anasema kuwa aliogopa kuripoti vitendo vya mumewe kwa kuwa alikuwa akimtishia yeye na wanawe uhai wao na alikuwa akiwanyanyasa kwa kuwapiga .
Waendesha mashtaka wamedai kuwa Aswad alianza kufanya ngono na mtoto wake mkubwa wakati akiwa na umri wa miaka nane na alimpa mimba mara nne huku akijifungua watoto mara zote nne.
Aswad anakumbukwa kwa video ya kundi la Hip-Hop la The Fugees ambao aliwatengenezea video ya wimbo wa Killing Me Softly na kupata tuzo ya Video Bora ya MTV  mwaka 1996.

Read more: http://audifacejackson.blogspot.com/2013/07/mfahamu-director-wa-video-aliyehukumiwa.html#ixzz2aahTADLZ

0 comments:

Post a Comment