Blogger Widgets

Monday, July 8, 2013

WASANII WAKUBWA DUNIANI WALIOBADILISHAJI SURA NA MAUMBILE YAO HAWA HAPA

Tina Turner
Tina Turner alifanyiwa upasuaji wa pua ambapo mwenyewe amekubali hilo.Hiyo ilikuwa ni kutokana na na manyanyaso na kipigo alichokuwaakipata kutoka kwa mumewe Ike na kusababisha mfupa wa pua kuvunjika na hivyo kupelekea yeye kufanyiwa upasuaji huo.Kuna habari za chini chini kuwa amefanyiwa upasuaji wa kunyanyua ngozi ya uso wake kwasababu licha ya kuwa na umri mkubwa Tina anaoneka mrembo bado!

Joan Rivers
Joan Rivers amefanyiwa upasuaji mara nyingi kurekebisha sura yake.Amesema kwa sasa hahitaji kufanyiwa upasuaji tena!


Madonna
Madonna amefanya marekebisho katika uso wake. Kaka yake Madonna alikubali kuwa Madonna alifanya upasuaji wa kunyanyua ngozi ya uso wake kiasi kumfanya yeye(kaka yake),kushindwa kumtambua Madonna.


Mel B

Nyota wa iliyokuwa Spice Girls Mel B ana umbo lenye mvuto.Nyota huyu alifanyiwa upasuaji kuongeza ukubwa wa matiti yake.Uongezwaji wa matiti ulimletea matatizo na kuamua yaondolewe. Pamoja na hivyo Mel B bado anaonekana ni mrembo


Michael Jackson
Mengi yaliandikwa kuhusu marekebisho yaliyofanyika katika uso na ngozi ya nyota huyu.Inasadikiwa kuwa Michael alifanyiwa upasuaji mara kadhaa kupunguza ukubwa wa pua yake!Rangi ya ngozi yake nayo ilibadilika kama picha ionyeshavyo!



Tina Turner
Tina Turner alifanyiwa upasuaji wa pua ambapo mwenyewe amekubali hilo.Hiyo ilikuwa ni kutokana na na manyanyaso na kipigo alichokuwaakipata kutoka kwa mumewe Ike na kusababisha mfupa wa pua kuvunjika na hivyo kupelekea yeye kufanyiwa upasuaji huo.Kuna habari za chini chini kuwa amefanyiwa upasuaji wa kunyanyua ngozi ya uso wake kwasababu licha ya kuwa na umri mkubwa Tina anaoneka mrembo bado!

Queen Latifah
Kutokana na maimivu ya mgongo na mabega aliyokuwa nayo Queen Latifah,ilimpelekea afanyiwe upasuaji kupunguza ukubwa wa matiti yake hivyo Queen Latifah alifanyiwa upasuaji si kwaajili ya sababu za urembo!



Jermaine Jackson
Siyo siri kuwa Jermaine Jackson amefanyiwa upasuaji wa kurekebisha pua na marekebisho katika ngozi yake.Habari zake zimekuwa zikiandikwa sehemu tofauti kwa muda sasa.

Idadi ya wasanii na matajiri waliofanya urekebishaji wa sura na ngozi zao ni kubwa na hawa ambao Sophie Mbeyu Blog imewatoa leo ni baadhi tu.Jamani,pesa zisitufanye tukamkufuru Mungu kwa kuikosoa kazi yake.Haya,ona wengine wameongeza maziwa,mara yanawasumbua wanaamua kuyatoa.Wengine ngozi zimebadilika kiasi ambacho unaweza kumpita mtu!
Tumeona watu wakijichubua na kuwa katika mwonekano wa kutatiza.Tumeona wengine wakiongeza makalio na kupata maumbo ya kutisha.Tujifunze kwa waliopata madhara na marekebisho ya miili yao na tufurahie kuishi katika mwonekano Mungu aliotupa!

0 comments:

Post a Comment