Blogger Widgets

Wednesday, July 31, 2013

Wasanii wajitolea kwenda kujenga kabuli la Bibi Kidude


Bi-Kidud2e
Bibi Kidude mkongwe wa muziki Tanzania ambaye alifariki huko Zanzibar na kuzikwa visiwani hapo, kifo chake kilipata maombolezo ya watu tofauti tofauti pamoja na wasanii. Hivi sasa wasanii wa kizazi kipya wamejiunga pamoja kwenda kusimamia swala zima la kujenga kabuli la mkongwe huyu katika historia ya muziki Tanzania. Msafara wa wasanii hadi sasa unategemewa kwenda Zanzibar siku ya Jumamosi hii kukamilisha mpango huu.
Bibi Kidude alipewa heshima ya pekee kwa kupata kumbukumbu ya heshima kwenye tamasha la Ziff ambalo lilifanyika Zanzibar kwa wasanii kuimba nyimbo zake kwenye stage kubwa ya ZIFF. Msanii Linah ambaye alirudia wimbo wa Yalaiti akiwa na Mwana F.A aliperform wimbo huu kwenye kumbukumbu hiyo.

0 comments:

Post a Comment