Blogger Widgets

Monday, July 8, 2013

TAARIFA YA MWEZI WA RAMADHAAN 1434H

Assalaamu 'alaykum wa Rahmatullaahi wa Barakaatuh,
 
Tumefuatilizia sana kila pahali taarifa za mwezi, na hatujapata taarifa zozote za mwezi kuonekana popote duniani leo Jumatatu 29 Sha'baan 1434H (8 Julai 2013M). Hivyo, kesho Jumanne tunakamilisha siku thalathini za Sha'abaan  In shaa Allaah, na Jumatano (10 Julai 2013M) itakuwa ni siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhaan.
 
ALHIDAAYA inawaombea Ramadhaan ya kheri na baraka nyingi, mchume thawabu tele, Swawm zikubaliwe, dhambi zighufuriwe, na Allaah Atutakabalie 'amali zetu.  Tusiache kuwaombea du’aa ndugu zetu Waislam popote walipo ulimwenguni walio katika dhiki za ukandamizwaji,
  vita, njaa na machafuko. Na pia tukumbukane kwa du’aa kwani Mtume Swalla-Allaahu alayhi wa aalihi wa sallam amesema katika Hadiyth kutoka kwa Ummu Dardaa (Radhiya-Allaahu ‘anhaa): ((Atakayemuombea ndugu yake kwa siri Malaika aliyewakilishwa kwake husema: “Aamiyn nawe pia upate mfano wake)) (wa kama unayomuombea) [Muslim]
 
Kwa Munaasabah wa kuukaribisha mwezi mtukufu wa Ramadhaan, Alhidaaya imewaekea tayari  mafundisho mbalimbali yenye manufaa katika kuongeza elimu na kuimarisha 'ibaadah zenu ili muweze kuchuma mema mengi na muweze kufikia kuipata taqwaa ambayo ndio lengo kuu la Swawm.

Read more: http://audifacejackson.blogspot.com/2013/07/taarifa-ya-mwezi-wa-ramadhaan-1434h.html#ixzz1qRyJ3l8g

0 comments:

Post a Comment