Blogger Widgets

Tuesday, July 30, 2013

SAKATA LA MADAWA YA KULEVYA IDD AZAN AFUNGUKA: “WANACHAMA WA CCM WANANICHAFUA”


Siku chache zilizopita mbunge wa Kinondoni Mh Idd Azan aliandikwa kwenye vyombo vya habari tofauti tofauti kwamba 
anajiusisha na madawa ya kulevya.
Chanzo za tuhuma hizo ni barua iliyoandikwa na mtanzania aliekamatwa huko china kwa kosa la kusafirisha madawa ya kulevya. Ndani ya barua hiyo Mh Idd Azan alitajwa kama kigogo ambaye anashughulika na biashara ya madawa ya kulevya. 
Siku ya jana Mh Idd Azan alifanya mahojiano na radio ya Clouds Fm na kusema kwamba tuhuma hizo ni za uwongo na hiyo barua pia ni ya uwongo.
Mh Idd Azan aliendelea kwa kusema kwamba wanachama wa CCM wanajaribu kumchafua kwa sababu wanajua uchaguzi unakaribia. Idd Azzan aliwataka wananchi wote wa kinondoni kutozitilia maanani habari hizo potufu zisizo na misingi yoyote.

0 comments:

Post a Comment