Blogger Widgets

Sunday, July 28, 2013

Yule shabiki wa Yanga alielia ilipofungwa 5 si akajitokeza kwenye BSS juzi, hizi ni picha alipolia baada ya kuambiwa hawezi

7 

3

1 
Tanzania ilimfahamu Steven baada tu ya kuonekana kwenye mahojiano ya Clouds TV akilia kutokana na Yanga kufungwa zile goli tano na Simba huku akidai zilikua hujuma, yani refa aliwapendelea Simba.

  Hapa katikati zilipita stori nyingi kumuhusu Steven, aliongea na millardayo.com na kusema baada ya kuonekana vile Mwenyekiti wa Yanga Yusuf Manji alimzawadia pikipiki kutokana na kuona uzalendo wake, alisema pia mpaka April 2013 alikua amepokea zaidi ya milioni 4 za Kitanzania kutoka kwa Watanzania mbalimbali ambao walimuona akilia.  Sasa Steven amemiliki headlines tena kwa kulia muda mfupi tu baada ya kushiriki usahili wa shindano la kusaka vipaji vya kuimba la Bongo Star Search July 27 2013 Uwanja wa Taifa Dar es salaam ambako anadai alijibiwa kwamba hana kipaji cha muziki hivyo akaendelee tu kuishangilia Yanga.  Video ya kulia kwake na kuimba utaiona baadae hapahapa millardayo.com ila kwa sasa nakupa nafasi uone hizi picha zake akiwa kwenye pozi mbalimbali baada ya kutoswa na Majaji…


4

5

6

0 comments:

Post a Comment