Blogger Widgets

Tuesday, July 30, 2013

Interview ya TV ya staa huyu, Yawa gumzo baada ya kuingia akiwa amevaa vazi la bafuni

Mkali wa filamu maarufu za Die Hard, Bruce Willis amekuwa gumzo katika media kutokana na safari hii kuamua kutokea katika mahojiano ya TV akiwa amevalia taulo - bathrobe kama moja ya 'mitupio' /vazi lake, na hivyo kuvunja mtazamo uliozoeleka na watu hususan mastaa, wa kujipanga saana kimavazi pale wanapokuwa wana mchongo wa interview ya TV.

Mtoko huu wa Bruce ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 58 ulikuwa ni katika  kipindi maarufu cha televisheni huko UK ambacho kinafahamika kwa jina 'Daybreak' cha mtangazaji maarufu KateGarraway.


Tazama picha za tukio hili hapa;

Bruce ambaye ni Baba wa mabinti wanne, Mabel 15, LaRue 22, Tallulah Belle 19, Rumer 24, kutokana na aina ya maisha anayoishi na familia yake hii ya mabinti, ametajwa kama moja ya mzazi na mwanafamilia bora, Tofauti kabisa na tabia za ugomvi na ukorofi anazohusishwa nazo na wengi hasa kutokana na aina ya filamu anazoshiriki.

0 comments:

Post a Comment