Blogger Widgets

Wednesday, August 14, 2013

HIKI MDICHO LULU NA MAMA AKE KANUMBA WAMEAMUA KUKIFANYA KWA PAMOJA






Elizabeth Michael(Lulu) ambaye ni muigizaji maarufu wa filamu ameanza kuwa active rasmi kwenye tasnia ya filamu kama mwanzo kwa kuanza kutengeneza films akiwa kama producer na pia muigizaji kama kawaida. Lulu kwasasa anashuti filamu ya Mapenzi Ya Mungu akiwa na Mama Kanumba, Linah na waigizaji wengineo huku yeye akiwa ndiye producer wa filamu hiyo. Huko nyuma alitengeneza filamu ya Foolish Age ambayo pia inatarajiwa kuingia sokoni muda si mrefu na ilichelewa baada ya Lulu kupata misukosuko kuhusiana na kifo cha Kanumba ambapo pia ilibidi asicheze filamu kwanza baada ya kuwa segerea kwa miezi kadhaa kabla ya kupata dhamana

Ukichilia mbali hilo inadaiwa kwasasa baadhi ya waandaji wa filamu tayari wameanza kumtaka Lulu katika filamu zao baada ya kurudi rasmi kwenye game kama awali. Lulu ni muigizaji mwenye mashabiki wengi katika filamu ukiachilia kipaji chake na hivi karibuni alipata tuzo ya muigizaji bora wa kike kutoka Zanzibar International Film festival(ZIFF). Hivyo wapenzi wa Lulu kaeni mkao wa kula kuona cheche zake on screen kama kawaida.

0 comments:

Post a Comment