Blogger Widgets

Monday, August 19, 2013

washauriwa kujihusisha na kilimo

Na Andrea ngobole,Arusha
 
NAIBU katibu mkuu wa jumuiya ya Africa Mashariki (EAC),Jesca Eriyo ametoa wito kwa vijana wa jumuiya hiyo kuweza kujituma na kujikita katika kilimo cha kisasa ili kiweze kuwakomboa na wimbi la umaskini linalowakabili vijana hapa Nchini

Eriyo alitoa rai hiyo  mwishoni mwa juma wakati akizundua kongamano la vijana wa jumuiya hiyo,katika ukumbi wa Light in Afrika uliopo wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro,lililoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la Vission for Youth lenye makao yake makuu  Mkoani Arusha na kukutanisha vijana 120 kutoka nchi wanachama.
 
Aidha  alibainisha kuwa ili kijana aweze kujikwamua kimaisha inamlazimu kujikita katika sekta ya kilimo cha kisasa ambapo jumuiya imeamua kuwaunga mkono vijana kwa kutoa fursa ya kuwatafutia masoko katika nchi wanachama ili waweze kuvuka mipaka na kujitangaza kupitia biashara wanazozifanya.

Alisema  kuwa vijana wanatakiwa kutambua kuwa kilimo ndiyo sekta pekee ambayo inaleta ajira ya moja kwa moja kwa kijana na familia kwa ujumla,kwani kilimo  ndiyo uti wa mgongo wa Taifa,kwani hivi sasa kilimo huliingizia pato Taifa kwa asilimia kubwa huku akibainisha kuwa kilimo hapa Nchini kinategemewa na wananchi kwa asilimia 75.
 
 
“mkitumia kilimo cha kisasa mtapata faida kwani kwa kutambua mchango wa kilimo Jumuiya ya Afrika mashariki imeweka mipango mathubuti ya kuwatafutia masoko katika nchi wanachama kwa kuondoa vikwazo vya ushuru barabarani na katika mipaka ya kutokea kutoka nchi moja kwenda nchi nyingine”alisema Eriyo
 
Aidha alisema ili vijana waeze kufankiwa wanatakiwa kuepuka  kutumia madawa ya kulevya (unga) ambayo yamekuwa yakiwadhoofisha afya na kukosa nguvu ya kutimiza ndoto zao ,kwani kijana akitumia madawa hayo anaweza kuathirika na  magonjwa ya kuambukiza ikiwemo Ukimwi na magonjwa ya mengine.
 
Alisisitiza pia kuwa vijana waliopo vijijini wanaweza kunufaika na soko la pamoja katika jumuiya hiyo,kwa kuuza bidhaa zao nje ya nchi,kwani miundo mbinu imeboreshwa katika nchi wanachama wa jumuiya ya hiyo,kuanzia mawasiliano ya simu,barabara, na kutolazimika kuwa na kibali cha kazi katika nchi wanachama.
 
Awali akimkaribisha mgeni rasmi katika ufunguzi huo,Afisa miradi wa shirika la Vission for Youth Vedastus Sibula,alisema changamoto inayowakabili vijana kwa hivi sasa ni kuogopa kutumia fursa zinazopatikana katika jumuiya hiyo,hivyo kwa kutambua hilo wameamua kuandaa kongamono la siku tatu,likishirikisha vijana kutoka Amerika,Uingereza,Tanzania, Uganda na Kenya likiwa na lengo la kuwapa fursa za zinazoweza kuwainua katika sekta ya kilimo cha kisasa.
 
MWISHO.

0 comments:

Post a Comment