Blogger Widgets

Monday, August 19, 2013

Wanaotuhumiwa kuwasaidia Agnes Masogange na mdogo wake kupitisha ‘Unga’ JNIA sasa kujieleza mbele ya tume

Mamlaka ya viwanja vya ndege Tanzania (TAA) imeanza kuchukua hatua dhidi ya wafanyakazi wanaotuhumiwa kuwasaidia Agnes ‘Masogange’ Gerald na mdogo wake Melisa Edward kupitisha dawa za kulevya katika uwanja wa JNIA (July 5).
madawa
Hatua hiyo inafuatia agizo la Waziri wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe aliyeitaka Mamlaka hiyo kuwachukulia hatua za kisheria wale wote waliohusika kula njama ya upitishwaji wa dawa hizo aina ya Crystal Methamphetamine, zilizoenda kukamatiwa katika uwanja wa ndege wa OR-Tambo, Afrika Kusini.

Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Julius Nyerere (JNIA), Moses Malaki, amesema wafanyakazi wanaotuhumiwa kula njama hiyo watasimamishwa kazi wakati wowote kuanzia leo kabla ya kupewa nafasi ya kujitetea kwenye tume itakayoundwa kuwachunguza.

Malaki ambaye awali alionyesha kushangazwa na kiasi kikubwa cha dawa hizo kupita, alisema utaratibu unakamilika wa kuundwa tume na kuwasimamisha kazi wahusika.

“Baada ya tume kukamilika na kupewa hadidu rejea, tutawaita mmoja mmoja kwenye kujieleza, hapo tutajua kama wahusika watakuwa na hatia au la,” alisema.

Alisema baada ya kumaliza kazi, tume itatoa maelekezo kwa Serikali kinachotakiwa kufanyika.

Ijumaa iliyopita (August 16) Dk. Mwakyembe alizungumza na waandishi wa habari kuelezea jinsi dawa hizo zilivyopitishwa uwanjani hapo, na kuiagiza TAA kuwafukuza kazi mara moja wafanyakazi wake wanne waliohusika katika mpango huo, kisha kuwakamata na kuwaunganisha katika mashitaka yanayowakabili.

SOURCE: MWANANCHI

0 comments:

Post a Comment