Blogger Widgets

Sunday, August 11, 2013

Nay wa Mitego na mchumba wake hapatoshi



Hatujathibitisha bado lakini tunahisi kuna ‘Tatizo’. Kupitia account yake ya Instagram Nay wa Mitego amekuwa akiandika ujumbe wenye mafumbo baada ya kuusoma ndani ya mistari (read between the line) tumegundua huenda mambo si mazuri kati yake na mpenzi wake ambaye hivi karibuni alikuwa akitarajia kumzalia mtoto lakini mimba ikaharibika.

Nay ambaye jina lake halisi ni Emmanuel Munisi, ameanza kwa kuandika ujumbe huu: Sasa mapenzi basi# by diamond Platnumz..!! Single boy# Ally Kiba#966’

Baada ya muda kidogo ameandika tena:

Niko ivi,,, nikikupenda nakupenda kwa asilimia 100# na kila m2 atajua juu ya upendo wangu kwako..!! Bt ukizingua nakuacha na ninakusahau kwa asilimia 200# na kwa muda mchache 2. Nikiamua huwa sirudi nyuma..!!# Mwanamke mjinga ataivunja ndoa yake kwa mikono yake ye mwenyewe# by Linex.#966’

Tunahisi mambo si mazuri kwenye ulimwengu wa mapenzi wa Nay, Itafahamika.

chanzo: http://shiladeux.blogspot.com

0 comments:

Post a Comment