Blogger Widgets

Monday, August 26, 2013

Ney wa Mitego afichua siri ya Diamond

MWIMBAJI bora wa Hip Hop 2013, Ney wa Mitego, ameweka wazi siri ya urafiki wake na msanii wa muziki wa kizazi kipya, Nassibu Abdul ‘Diamond’. Ney wa Mitego amesema Diamond ni shemeji yake kwa kuwa mchumba anayetarajia kumuoa aliyemtaja kwa jina la Siwema, ni mzaliwa wa Mkoa wa Kigoma anakotokea msanii huyo.

“Mchumba wangu ambaye anapagawa zaidi na kibao changu cha ‘Hero’ kuliko nyimbo nyingine zote nilizowahi kuimba ni dada yake Diamond, kwa kuwa wanatoka mkoa mmoja, hivyo ni shemeji yangu,” alisema.


Mkali huyo wa Hip Hop amesema Diamond ni rafiki na shemeji yake, lakini pia mchumba wake (Siwema) ni zaidi ya mpenzi kutokana na kuwa mshauri mkubwa katika muziki anaoufanya, ambapo anazikubali nyimbo zote alizoimba, japokuwa kibao cha Hero kinampagawisha zaidi.


CHANZO: Mwananchi.

0 comments:

Post a Comment