Blogger Widgets

Wednesday, August 14, 2013

Janjaro: Naipenda Tip Top Connection lakini siwezi kurudi ng’o (Audio)

Rapper wa kundi la Mtanashati Entertainment, Dogo Janja aka Janjaro amekanusha madai ya Babu Tale kuwa amekuwa akimpigia simu Madee ili wakae kuongea na kumaliza tofauti zao.
1014172_700831366609934_2041385663_n
Dogo Janja amesema anawaheshimu Tip Top kama wazazi wake lakini kamwe hafikirii kujiunga tena na kundi hilo.
“Mimi kama mimi, kumtafuta, naweza nikampigia simu, nikamsalimia, Babu Tale naweza nikamtafuta nikamsalimia wote nikaongea nao sababu hizi ni beef za kibiashara sio beef za sio za kibinadamu kwahiyo sina beef nao. Sio kwamba mimi eti nimpigie simu Madee kwamba tuyamalize nirudi Tip Top hapana, mimi kurudi Tip Top siwezi na mimi nawapenda, nawaheshimu kama brother zangu, kama wazazi wangu kwenye huu muziki. Lakini mimi nipo Mtanashati na nitaendelea kuwa Mtanashati,” amesema Janjaro.

Msikilize zaidi hapa.

0 comments:

Post a Comment