Blogger Widgets

Tuesday, August 20, 2013

Lady Jaydee atoa siri tano nzito...!!!

Mwanadada Judith Wambura aka Lady Jaydee, amefunguka kwa kutoa njia tano zinazoweza kumfanya mtu aweze kufika kwenye mafanikio katika jambo alifanyalo.
404501_10151250606915025_800711642_n
Jaydee amekuwa akiulizwa maswali katika ukurasa wake wa Facebook kuhusiana na njia zinazoweza kumfanya mtu afanikiwe katika shughuli anayoifanya na kwakuwa wengi humwamini yeye kama kioo cha jamii anayeweza kuwa mfano wa kuigwa.
Siri alizozitaja ni pamoja na:
1. Kujiamini Kutoogopa, kuthubutu kufanya kile unachoamini unaweza.
2. Kuipenda kazi unayoifanya hata kama ina kipato kidogo.
3. Kufanya maamuzi sahihi bila kuangalia pembeni.
4. Kuenda kuchukua chako bila kusubiri kuletewa.
5. Kufanya kazi kwa bidii bila kuchoka.


source bongo 5

0 comments:

Post a Comment