Blogger Widgets

Tuesday, May 21, 2013

HIVI NDIVYO MADEE ALIVYOMPONGEZA DOGO JANJA




Na Elizabeth John

KIONGOZI wa Kundi la Tip Top Connection, lenye maskani yake Manzese jijini Dar es Salaam, Ahmed Ally ‘Madee’, amesema amevutiwa na kazi ya msanii nyota katika muziki wa kizazi kipya nchini, Abdulazizi Chende ‘Dogo Janja’ inayoendelea kufanya vyema katioka vituo mbalimbali vya radio.



Kauli hiyo imekuja baada ya wapenzi wa muziki huo, kufikiria kwamba Madee angeichukia ngoma hiyo ya Dogo Janja inayokwenda kwa jina la  ‘Ya Moyoni’ kwa kuhisi kuwa imemzungumzia yeye lakini haijawa hivyo.



Akizungumza Dar es Salaam jana, Madee alisema kuwa bado ni shabiki mkubwa wa Dogo Janja na anampongeza sana kwa kufanya vizuri na ngoma hiyo inayoendelea kufanya vyema katika vituo mbalimbali vya radio.



Madee alisema amependa zaidi kiitikio kilichofanywa na PNC lakini ameongeza kuwa kama angeisikia kabla ya kupelekwa redioni angependekeza yafanyike marekebisho kadhaa.



Miezi kadhaa iliyopita Madee na Dogo Janja walikuwa gumzo kwenye vyombo vya habari vya Tanzania baada ya Madee kushutumiwa kumtumia msanii huyo isivyotakiwa kiasi cha kufanya aondoke katika kundi hilo.

0 comments:

Post a Comment