Blogger Widgets

Wednesday, May 15, 2013

PICHA YA LEO: HIVI NDIVYO LADY JAYDEE NA MME WAKE WALIVYOKWENDA MAHAKAMANI, LIKE BEYONCE NA JAY Z

MWANAMUZIKI Mahiri wa Bongo Fleva, Judith Wambura 'Lady Jaydee' alifika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam kufuatia kufunguliwa kesi ya madai katika mahakama hiyo. Katika hati ya madai hayo, mwanamuziki huyo anashitakiwa na viongozi wa Clouds Media Group ambao ni Ruge Mutahaba na Joseph Kusaga. Tuhuma za kesi hiyo zinatarajiwa kusomwa mahakamani hapo na Hakimu, Athuman Nyamrani Mei 27 mwaka huu. Jaydee aliwasili mahakamani hapo akiwa na mumewe Gadner G. Habash mishale ya saa 6 mchana na kuongoza moja kwa moja chumba cha makarani wa mahakama hiyo ambao aliwakabidhi hati ya mashitaka hayo.

0 comments:

Post a Comment