Blogger Widgets

Tuesday, May 28, 2013

Nay Wa Mitego atoa siri ya kwanini huvaa viatu vya pair mbili tofauti!

nay

Kuwa na ‘unique identity’ ni moja ya technics nzuri kibiashara kwa msanii sababu inafanya atambulike kirahisi na kwa haraka miongoni mwa wasanii wengi.
Hakuna ubishi kuwa baba kijacho Nay Wa Mitego is running the game right now, kupitia hit song aliyoshirikiana Diamond Platnumz.
Nay amekuja na style yake ya kuvaa viatu viwili vya pair mbili tofauti na ndivyo anavyoonekana mara zote anapokuwa popote iwe ni kwenye show au mtaani. Kama bado unashangaa au hujaelewa ni hivi, mfano anakuwa na pair mbili za viatu lets use Adidas na Puma, pair moja iwe nyeupe na nyingine nyeusi, mguu mmoja anavaa Adidas nyeupe na mguu mwingine anavaa puma nyeusi, that’s his new swag, sio uchawi lakini!!
Kris-Kross
Akiielezea style yake hiyo ya uvaaji viatu kupitia kipindi cha Hot Mix cha EATV Nay amesema “navaa hivi nikimaanisha binadamu hatufanani, wewe huwezi kuwa sawa na yule na mi siwezi kuwa sawa na wewe that’s the big point”.
Wapo wasanii wengine wa nje na hapa Tanzania ambao wamewahi kujaribu kufanya vitu vya kuwatofautisha na wengine. Mfano kwa nje kundi la Kriss Kross wao style yao ilikuwa ni kugeuza jeans mbele kuwa nyuma na nyuma kuwa mbele.
Mpoto
Hapa Tanzania mwana mashairi Mrisho Mpoto ana aina yake ya mavazi anayovaa muda mwingi yanayomtambulisha na pia mara kadhaa huwa anatembea peku bila viatu.

0 comments:

Post a Comment