Blogger Widgets

Thursday, February 21, 2013

ANGALIA SHULE HII ILYOFUNGIWA, KWA MTINDO HUU ZERO LAKI MBILI ZITAACHA KUWEPO?

Mkuu wa wilaya ya Ilemela Amina Masenza akishuhudia mrundikano wa magodoro sehemu wanayolala wavulana wa shule ya Mount Zion kwenye moja ya vyumba vya darasa vilivyotengwa kwa ajili ya kujisitiri.
Vyoo vilivyobananishwa ndani ya bweni pembeni yake kuna masanduku ya nguo ya Wanafunzi.
Hawa Wanafunzi walifichwa na mwalimu wa shule hiyo baada ya kusikia Mkuu wa Wilaya anakuja kufanya ukaguzi wa ghadla kwenye hiyo shule.
Wanafunzi wa kidato cha kwanza waliojificha na mwalimu wao wakirudishwa shuleni, lengo la kujificha ilikua ni kukwepa kukutwa wamekalia ndoo kwenye msongamano madarasani.
Mkuu wa Wilaya ya Ilemela akizungumza huku machozi yakimlenga kutokana na alichokiona shuleni hapo,  aliagiza hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya Mkurugenzi wa shule hiyo ya Mount Zion Ilemela.
.
Shule ya Sekondari ya Mount Zion ina jumla ya vyumba 7 vya madarasa ambavyo ilisajiliwa navyo kuhudumia wanafunzi 160 lakini sasa hivi wanafunzi wameongezeka na kufikia 515 ambapo madarasa mengine yana wanafunzi mpaka 119 na wengine wanakalia ndoo badala ya viti.
.
.
Kingine kilichogundulika ni kwamba Wanafunzi wanaosoma hapa wengi wanatoka mikoa mbalimbali ambapo huyu mjumbe aliwauliza na wanafunzi kumjibu Mikoa waliyotajaambayo ni Shinyanga, Mara, Kagera, Dodoma, Mbeya, Morogoro, Tanga na hata Dar es salaam wapo.
.
Nje ya Hostel.
Wanalala hapa, tazama jinsi hata walivyoweka vyandarua
.
Ni ndani ya moja ya vyumba vya wasichana ambacho ndani yake kuna matandiko haya na masanduku 13 ikimaanisha ndiyo idadi ya wasichana wanaolala hapa.
Chumba kingine cha Wasichana.
Akiwa amepakizwa kwenye pikipiki kuelekea zahanati ya jeshi iliyo karibu na eneo la shule, mwanafunzi huyu aliyekuwa hoi akiumwa na alikutana njiani na msafara wa kamati ya ulinzi na usalama ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya Ilemela Amina Masenza ambae aliagiza moja kati ya magari kwenye msafara wake kumpeleka hospitali.
Aliingizwa humu.
Baada ya mapungufu mengi kuonekana ikiwa ni pamoja na kukosa mabweni, Idara ya Afya Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela Mwanza imetoa agizo la kisheria kuifungia mara moja shule ya Sekondari ya Mount Zion kutokana na kukiuka kanuni za uendeshaji wa shule pamoja na shule hiyo kukithiri kwa uchafu.

Ripoti hii imeandaliwa na mwandishi Albert G Sengo ambae pia ni mmiliki wa gsengo.blogspot.com

0 comments:

Post a Comment